Ugonjwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Unene wa kipindukia ulitazamwa kama dalili ya cheo katika jamii nyingi lakini leo hii hutazamwa kama ugonjwa

Ugonjwa ni hali ya mvurugo katika utendaji wa kawaida wa shughuli za mwili na roho inayoathiri vibaya starehe ya kiumbehai. Hakuna tofauti kamili baina ya ugonjwa na hali ya kujisikia vibaya.

Sayansi inachochungulia magonjwa ni tiba

Siku hizi magonjwa hupangwa kufuatana na sababu zao kama vile

  • magonjwa ya kuambukizwa
  • magonjwa ya kurithiwa
  • magonjwa kutokana na ajali
  • magonjwa kutokana na dutu za nje ya mwili (sumu, asidi ) au moto
  • magonjwa ya kansa
  • magonjwa yaliyosababishwa na tiba
  • magonjwa yaliyosababishwa na mfumo wa kinga mwilini
  • magonjwa ya roho