Vielezi vya idadi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mifano
  • Mjomba ana hasira kiasi kidogo
  • Kaibiwa mara mbili sasa


Vielezi vya idadi au kiasi (alama yake ya kiisimu ni: E) ni maneno yanayofafanua kielezi kuwa kitenzi hicho kitemetendeka mara ngapi au kwa kiasi gani. Idadi hiyo inaweza kuwa idadi ya jumla au idadi kamili/halisi.

Uchambuzi[hariri | hariri chanzo]

Mifano
  • Mtoto huyu amepigwa mara nne (mtoto = nomino ya kawaida, huyu = kivumishi cha kuonesha, amepigwa = kitenzi kikuu, mara nne = kilezi cha idadi au kiasi kamili au halisi ya huyo mtoto kupigwa kwake).
  • Kamanga hula mara chache (Kamanga = nomino ya pekee, hula = kitenzi kikuu, mara chache = kielezi cha idadi au kiasi cha jumla - jumla kwa maana hakuna namba kamili au idadi kamili-halisi iliyotajwa hapo).
  • Husna ameanguka mara nyingi
  • Chakula kimepikwa mara mbili
  • Nyumba imeanguka mara tatu

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vielezi vya idadi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.