Kitenzi kikuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mifano
  • Kawaida yetu kukimbiza maisha ya kila siku
  • Kijana anakula chakula cha jana
  • Dada kachoka kutembea
  • Mlinzi analinda eneo lake la kazi
  • Gari lako linakwenda mbio sana

Kitenzi kikuu (alama yake ya kiisimu ni: T) ni kitenzi ambacho hutoa wazo kwa tendo ambalo linatendwa na nomino au kiwakilishi cha nomino. Mara nyingi kitenzi kikuu hukaa peke yake katika sentensi na hutoa taarifa kamili bila ya kuhitaji msaada wa kitenzi kingine.

Mifano
  • Babu yangu analima shambani
  • Shamba letu limepandwa migomba
  • Juma ameandika barua ya kuomba kazi
  • Chakula kimepikwa vizuri
  • Sisi tunasoma somo la Kiswahili

Sifa za kitenzi kikuu[hariri | hariri chanzo]

  • Huweza kusimama peke yake katika tungo au sentensi na kukamilisha taarifa bila ya kuwepo kitenzi kingine.

Mfano: Mama anakula

  • Huweza kuonesha ukanushi au uyakinishi

Mfano: Mimi ninakimbia (uyakinishi) Wewe hutaimba wimbo huu (ukanushi)

  • Huundwa kwa viambishi mbalimbali.

Mfano: Wa- ta- mu- on-a

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitenzi kikuu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.