Silabi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambapo sauti za lugha hutamkwa mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti.

Maneno kufanywa na silabi. Maneno mafupi huwa na silabi 1 pekee. Maneno mengine huwa na silabi zaidi kama 2, 3 au nyingi. Silabi fupi sana inaweza kuwa vokali 1 pekee au konsonanti 1 kama "m" katika "m-to-to".

Kama silabi inaishia kwa konsonanti inaweza kuitwa silabi iliyofungwa, kama inaishia kwa vokali inaweza kuitwa silabi wazi.

Kuna lugha zilizo na silabi nyingi zilizofungwa kama Kiingereza. Kiswahili kinapendelea silabi wazi, lakini "m" na "n" zinaweza kuwa mwishoni kwa silabi au kuwa silabi peke yao. Lugha kama Kijapani takriban hazina silabi za kufungwa.

Mifano ya maneno yenye silabi 1:

 • tu
 • na

Maneno mengi ya Kiswahili huwa na silabi mbili au zaidi:

 • ne-n-da
 • ku-ja
 • shu-le
 • hi-i
 • ma-a-na
 • ra-fi-ki
 • se-ko-n-da-ri
 • se-ri-ka-li
 • i-li-yo-fu-n-gwa

Kuna lugha zinazotumia mwandiko wa silabi badala ya alfabeti, kwa mfano abugida.