Nenda kwa yaliyomo

Kitenzi kikuu kisaidizi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mifano
  • Oliver 'hakutaka kula ugali
  • Habibu angali anasoma darasani
  • Sisi tunataka kwenda kuogelea mtoni

Kitenzi kikuu kisaidizi (alama yake ya kiisimu ni: TS) ni kitenzi ambacho hukaa sambamba na kitenzi kikuu ili kukisaidia kukamilisha taarifa. Kitenzi kikuu kisaidizi kikiwa peke yake hakiwezi kutoa taarifa kamili. Hivyo basi ni lazima kiambatane na kitenzi kingine (kikuu) ndipo taarifa yake ikamilike.

Uchambuzi

[hariri | hariri chanzo]
  • Babu yangu alikuwa anaumwa sana (alikuwa ni kitenzi kisaidizi TS - na anaumwa ni kitenzi kikuu T).
  • Wezi walikuwa wanataka kuiba fedha zake (walikuwa na wanataka vyote ni vitenzi visaidizi - isipokuwa kuiba ambapo hapa kimeainishika kama kitenzi kikuu). Kwa kawaida kitenzi kikuu hukaa mwisho hata kama nyuma yake kutakuwa na wasaidizi kumi.
  • Anna alikuwa anataka kwenda kununua matunda sokoni (alikuwa, anataka, na kwenda vyote ni vitenzi visaidizi isipokuwa kununua inabaki kuwa kitenzi kikuu
  • Upepo ulikuwa umesha ezua mabati yote
  • Juma hakuwa anataka kwenda kununua matunda sokoni

Angalizo: Kitenzi kikuu alama yake ni T kubwa na kitenzi kisaidizi alama yake ni TS.

Dhima za kitenzi kikuu kisaidizi

[hariri | hariri chanzo]

Dhima za kitenzi kikuu kisaidizi zimegawanyika katika makundi makuu mawili - nayo ni:

1) Kujulisha njeo (njeo = wakati, nyakati)

2) Kujulisha uyakinishi na ukanushi wa tendo/matendo

Sifa za Kitenzi kisaidizi

- Hakikamilishi taarifa. Mfano, Baba alikuwa

- Mara zote huambatana na kitenzi kikuu katika kutoa taarifa. Mfano, Upepo ulikuwa unavuma.

- Hudokeza nyakati mbalimbali za kutendeka kwa tendo. Yaani, wakati uliopo, uliopita na ujao. Mfano, Alikuwa, Atakuwa, n.k

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitenzi kikuu kisaidizi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.