Usanii

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Usanii

Usanii ni neno lenye maana pana sana. Kwa kifupi ni ubunifu wa vitu mbalimbali unaofanana na uumbaji.

Mtu anayejishughulisha na usanii huitwa msanii, na kile alichokibuni au kukiumba huitwa sanaa.

Wasanii wengi wanaamini kuwa Mungu ni msanii mkubwa wa kwanza, kwa sababu ndiye aliyeumba vitu vyote, ambavyo wasanii, hasa wa uchoraji, huviiga na kuvibadili kidogo. Hapa ndipo ubunifu unapochukua nafasi katika usanii.

Msanii kupitia vitu anavyoviumba, kama ni picha ya kuchora au muziki, hapo hupata nafasi ya kueleza hisia zake za ndani, k.mf. furaha, au ya wengine, huzuni yake au ya wengine, kuelimisha, au kufurahisha.

Msanii ni mtu muhimu sana katika jamii, kwa sababu kwa njia ya sanaa ni rahisi kufikisha ujumbe kwa watu wengi na kwa wakati mmoja, hasa sanaa ya uimbaji, yaani muziki. Sanaa ya uchoraji inachuka muda kufikisha ujumbe au burudani lakini ni sanaa inayotunza ujumbe au kuvutia kwa muda mrefu zaidi, kwa sababu watu wengi, hasa wa nchi za Afrika, bado hawana mwamko wa sanaa hiyo,ukilinganisha na nchi za Ulaya na Amerika, ambako sanaa hiyo inathaminiwa sana na watu wengi na marika yote.

Tofauti kati ya uimbaji na uchoraji ni kama ifuatavyo:

  • Ujumbe uliobebwa na usanii wa muziki hupita kwa muda mfupi au mrefu kutegemeana na aina ya muziki huo, kwa sababu watu hupokea aina nyingi za ujumbe kwa wakati mmoja, na pengine wanaweza wasisikilize tena muziki huo na wakasahau kabisa ujumbe ule, lakini sanaa ya uchoraji iliyoandaliwa kwa ustadi mkubwa, huisahau hudumu kwa miaka mingi sana, hivyo humpa nafasi mhusika kurudia kupata ujumbe kila anapotazama sanaa hiyo.

Hivyo sanaa hiyo pia ni muhimu sana kwa kutunza kumbukumbu, hasa pale msanii anapochora picha inayoonyesha hali halisi ya wakati fulani ambao hupita na watu kusahau, hivyo kwa kutazama picha au mchoro huo watu au jamii hupata kumbukumbu ya jambo au tukio au wakati huo uliopita.

Hii ni maana ya usanii au sanaa kwa kifupi, lakini siku hizi imetokewa na wezi wa maneno au kwa lugha rahisi matapeli kuitwa wasanii, kwa sababu wanabuni na kuumba maneno ya udanganyifu na kuyageuza kama ni ya ukweli ilhali si ya ukweli. Hii si sawa kabisa na wasanii wengi wanawataka watu waache kabisa kutumia neno hili kwa watu wa namna hiyo, na watu hao waitwe wezi au matapeli kama inavyofamika.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: