Nenda kwa yaliyomo

Ubunifu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mbunifu wa mitindo ya mavazi akionesha ubunifu wake

Ubunifu (kutoka kitenzi chenye asili ya Kiarabu "kubuni"; pia: ugunduzi, japo si maneno yanayolingana kabisa katika maana zake.[1] ) mara nyingi huchukuliwa kuwa ni matumizi ya njia bora zaidi zinazokidhi kutatua changamoto mpya, changamoto ambazo tayari zipo lakini hazijapatiwa ufumbuzi bado, au changamoto zilizopo kwenye soko au jamii kwa kipindi husika.[2]

Dhana hii hutimilika pale ambapo bidhaa, huduma, teknolojia, mpangilio wa biashara au njia nyingine yoyote inayoweza kutatua changamoto husika katika jamii ni adimu kuipata katika masoko ya kiuchumi, serikali au jamii yenyewe.

Neno ubunifu linaweza kutafsiriwa kuwa ni kitu fulani halisia na chenye mchango wa wazi katika jamii na hivyo ni kitu kipya kinachojitokeza katika soko au jamii kwa hali ya upya[3].

Ubunifu chanzo chake ni Mungu maana ndiye aliyeanzisha vitu vyote kwa kuachilia mawazo ndani ya watu.

Ili ubunifu uweze kuonekana ni lazima wabunifu waaminiwe, wapewe kipaumbele, ikiwezekana pia wapewe mitaji na kuendeleza elimu za ubunifu wao.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Bhasin, Kim (2012-04-02). "This Is The Difference Between 'Invention' And 'Innovation'". Business Insider.
  2. Maryville, S (1992). "Entrepreneurship in the Business Curriculum". Journal of Education for Business. Vol. 68 No. 1, pp. 27–31.
  3. Based on Frankelius, P. (2009). "Questioning two myths in innovation literature". Journal of High Technology Management Research. Vol. 20, No. 1, pp. 40–51.