Nakshi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nakshi ya Kiarabu juu ya kifaa cha Kituruki.
Sahani ya China yenye mchoro wa joka.

Nakshi ni kitu chochote kinachotumika kuongeza mvuto wa uzuri wa kitu fulani.

Toka zamani za kale binadamu ameonyesha kipaji chake cha usanii kwa kutia nakshi vitu mbalimbali alivyotengeneza au alivyotumia.

Nakshi zilitumika kwa namna ya pekee upande wa dini, katika maabadi na katika vifaa vya ibada, kama vile mavazi.