Misri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
جمهوريّة مصرالعربيّة
Gumhūriyyat Misr al-ʿarabiyya
Jamhuri ya Kiarabu ya Misri
Flag of Egypt.svg
Bendera ya Misri
Coat of arms of Egypt.svg
Nembo la Misri
Lugha rasmi Kiarabu
Mji Mkuu Cairo-Maadi
Serikali Jamhuri
Rais Abdel Fattah el-Sisi
Waziri Mkuu Ibrahim Mahlab
Eneo km² 1.002.450
Wakazi 90.000.000 (2015)
Wakazi kwa km² 84 kwa jumla; katika bonde la Nile 1120
Uhuru 26 Julai 1952 kutoka Uingereza
Pesa Lira au Pauni ya Misri = 100 Piaster
Wakati UTC +2
Wimbo ya Taifa Biladi, Biladi, Biladi (nchi yangu)
Egypt in its region (undisputed).svg
Ramani ya Misri

Misri (kwa Kiarabu: مصر, Masr) ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Mashariki ikiwa na eneo la Rasi ya Sinai kwenye bara la Asia pia.

Ni nchi yenye wakazi milioni 90 na mji mkuu Kairo ni kati ya miji mikubwa zaidi duniani.

Ni kati ya nchi ya dunia yenye historia ndefu inayojulikana.

Jina la nchi[hariri | hariri chanzo]

  • Jina la Misri kwa Kiswahili linalingana na jina rasmi la Miṣr katika lugha ya Kiarabu. Ni jina la Kale jinsi inavyoonekana katika Biblia ya Kiebrania ambako inaitwa Mitzrayim (מִצְרַיִם, wingi wa Misri kumaanisha Misri ya Juu na Misri ya Chini). Maana ya jina hili ni "nchi".
  • majina ya Kizungu ya "Egypt" (ing.), "Egypte" (far.), "Ägypten" (jer.) yanatokana na jina la Kigiriki Αίγυπτος (aigyptos). Hakuna hakika juu ya maana asilia ya neno. Wengine huamini neno limetokana na jina la hekalu muhimu mjini Memphis. Neno hili ni pia asili ya jina "Wakopti" na hii ni jinsi wenyeji wa Misri walivyojiita wakati wa utawala wa Dola la Roma

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Misri imepakana na Bahari ya Mediteranea, Israel, Eneo la mamlaka ya Palestina, ghuba ya Suez, ghuba ya Aqaba, Bahari ya Shamu, Sudan na Libya. Umbo la nchi hufanana na trapeza.

Tabianchi ni yabisi sana na maeneo makubwa ni jangwa, pamoja na oasisi na maeneo ya savana ya miiba. Karibu wananchi wote huishi ndani ya kanda nyembamba ya bonde la mto Naili. Bonde hili linavuka nchi kuanzia mpakani na Sudani katika kusini kuelekea kaskazini hadi mdomo wa mto kwenye Bahari ya Mediteranea. Ardhi pande zote mbili za mto inamwagiliwa na kulimwa. Kwatika umbali mdogo kutoka mto jangwa inaanza.

Takriban kilomita 250 kabla ya mdomo Naili inagawanyika katika mikono mbalimbali na kuunda delta ya mto.

Kanda hili bichi si zaidi ya asilimia 5 za eneo lote la nchi, ila 98% za wananchi wote huishi humo.[1] Kwa hiyo Naili huitwa "Baba wa Misri", kwa maana bila mto huo pasingekuwepo taifa hili.

Mji mkuu wa Kairo uko mwanzoni mwa eneo la delta.

Nchi yote huwa na kanda asilia zifuatazo:

  • Delta ya Naili: upande wa kaskazini wa Kairo Naili inajigawa katika mikono miwili mikuu na kati ya mikono hiyo miwili kuna eneo la delta yenye km² 23,000 kwa umbo la pembetatu. Inajaa ardhi ya rutuba kutokana na matope ya Naili iliyopelekwa huko na mafuriko katika muda wa miaka elfu kadhaa. Eneo hili linalimwa kote na kumwagiliwa likiwa na mikono midogo ya kando ya Naili.
  • Jangwa la Magharibi: ni eneo kubwa upande wa magharibi wa Naili lisilo na milima mikubwa. Kaskazini mwake kuna tambarare ya Lybia iliyo takriban mita 240 juu ya uwiano wa bahari. Kusini mwake linainama eneo la mbonyeo wa Qatara hadi mita 133 chini ya UB, halafu jangwa linapanda tena juu kuelekea kusini magharibi.
Ndani ya eneo hili kubwa kuna beseni kadhaa pamoja na oasisi za Siwa, Bahariyya, Farafra, Dakhla na Charga. Kilomita 100 upande wa kusini-magharibi wa Kairo kuna oasisi kubwa ya Fayyum pamoja na ziwa la Warun lenye eneo la km² 230.
  • Jangwa la Mashariki: ni eneo upande wa mashariki wa mto Naili. Huko kuna milima inayopanda juu ya mita 2,000 pamoja na wadi yaani bonde kali. Jangwa linatelemka hadi mfereji wa Bahari ya Shamu ambao ni sehemu ya Bonde la Ufa linaloanza Palestina na kuendelea hadi Ziwa Nyasa.
  • Rasi ya Sinai: ni eneo la jangwa na milima inayofikia hadi mita 2637 (Jabal Katharina).

Historia[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu: Historia ya Misri

Nchi hiyo ni kati ya vitovu vya ustaarabu wa binadamu, na kwa sababu hiyo inavutia watalii wengi.

Baadaye kwa karne nyingi Misri ilikuwa rasmi sehemu ya Milki ya Osmani lakini hali halisi ilisimamiwa na Uingereza hasa kwa shabaha ya kutawala mfereji wa Suez.

Mwaka 1914 ilitangazwa kuwa nchi lindwa chini ya Uingereza; tangazo la uhuru la mwaka 1922 bado liliacha athira kubwa kwa Uingereza.

Tangu mwaka 1952 Misri imepata uhuru kamili, na tangu hapo ilitawala pia mfereji wa Suez.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Msongamano (watu kwa kilometa mraba).

Wakazi wengi (91%) ni Wamisri asili.

Lugha rasmi ni Kiarabu Sanifu cha Kisasa, wakati wananchi wanatumia kwa kawaida aina mbalimbali za Kiarabu, hasa Kiarabu cha Kimisri (68%)

Upande wa dini, sheria zinazitambua 3 tu: Uislamu, ambao ndio dini rasmi, Ukristo na Uyahudi.

Uwiano wa wafuasi wa dini hizo haujulikani vizuri, lakini Waislamu (hasa Wasunni) ni kama 90%, Wakristo (hasa Wakopti wanaoendelea kufuata Ukristo uliokuwa unatawala kabla ya Waarabu kuteka nchi katika karne ya 7) ni kama 9%, wakati Wayahudi wamehama karibu wote.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Taarifa za jumla
Biashara
Mengineyo


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Misri kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. [ http://www.oceandocs.org/bitstream/handle/1834/383/Hamza.pdf;jsessionid=27AB61FA3D2E5414E61CED1F78061F86?sequence=1 Waleed Hamza : Land use and Coastal Management in the third Countries; Egypt as a case; http://www.oceandocs.org , imeangaliwa Machi 2016]