New Delhi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Jiji la New Delhi
Jiji la New Delhi is located in Uhindi
<div style="position: absolute; z-index: 2; top: Expression error: Unexpected < operator.%; left: Expression error: Unexpected < operator.%; height: 0; width: 0; margin: 0; padding: 0;">
Jiji la New Delhi
Jiji la New Delhi
Mahali pa mji wa New Delhi katika Uhindi
Majiranukta: 28°40′N 77°13′E / 28.667°N 77.217°E / 28.667; 77.217
Nchi Uhindi
Tovuti: http://www.ndmc.gov.in/
"India Gate" mjini New Delhi
Boma Nyekundu la Delhi ni jengo mashuhuri lililojengwa kwa Shah Jahan
Majengo ya serikali katika Delhi mpya yalijengwa na Waingereza

New Delhi (yaani Delhi Mpya; kwa Kihindi: |नई दिल्ली, kwa Kiurdu: نئی دلی) ni mji mkuu wa Uhindi na kitovu cha jiji kubwa la Delhi. Pamoja na Delhi yote kuna wakazi zaidi ya milioni kumi.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Iko katika kaskazini ya nchi kwenye kingo za mto Yamuna katika tambarare ya bonde la Ganga. Mji huo uko m 216 juu ya UB kwa wastani.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Delhi ina historia ndefu sana iliyoanza mnamo mwaka 1200 KK. Iliharibiwa mara nyingi na kujengwa upya na kubadilisha jina pamoja na wakazi na watawala wake. Katika karne zilizopita ilikuwa mji mkuu wa Dola la Moghul na tangu mwaka 1911 wa Uhindi wa Kiingereza.

Delhi Mpya ilianzishwa baada ya azimio la George V, mfalme wa Uingereza na Kaisari wa Uhindi, la kuhamisha mji mkuu kutoka Kalkutta kwenda Delhi. Mji mpya ulijengwa kando ya Delhi ya Kale na kukabidhiwa mwaka 1931. Ulisanifiwa na wasanifu Waingereza Edwin Lutyens (1869-1944) na Herbert Baker (1862-1946).

Tangu mwaka 1947 New Delhi ni mji mkuu wa Uhindi huru.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Map of Asian states.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu New Delhi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.