Tovuti
Mandhari
Tovuti (Kiing. website)[1] ni mkusanyiko wa kurasa zilizoandikwa kwa lugha mbalimbali za tarakilishi kama vile HTML, PHP, XHTML na kadhalika na ambazo kwa pamoja hujumuika katika kutoa habari au maelezo kuhusu jambo fulani. Lugha hizi, yaani HTML, PHP, XHTML na kadhalika zinaweza tu kusomwa na kutafsiriwa na programu kama vile Internet Explorer Google Chrome na Mozilla Firefox kwa lugha ambayo inaweza kueleweka na binadamu. Wingi wake ni "tovuti" vile vile. Tovuti zote pamoja zinaitwa "mtandao" au "Intaneti" au "wavuti".
Marejeo
- ↑ Hivyo Kamusi ya Kiswahili sanifu4 na Kamusi ya Kompyuta
Viungo vya nje
- Tovuti ya kwanza iliyoundwa na Tim Berners-Lee
- Internet Corporation For Assigned Names and Numbers (ICANN) - Shirika Linalosimamia Anuani za Tovuti Duniani
- World Wide Web Consortium (W3C) - Shirika Linalohusika na Kanuni za Msingi za Ujenzi wa Tovuti (na mambo mengine yanayohusika na tovuti)
- The Internet Society (ISOC)