Nenda kwa yaliyomo

Mjukuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mjukuu ni mtoto wa mwanao, bila kujali jinsia yako wala yake. Yeye anakuita babu au bibi.[1]

Mtoto wake tena anaitwa kitukuu, mtukuu au kusukuu.[1]

Katika Kiswahili ni maarufu mithali inayosema, "Majuto ni mjukuu", kwa maana mara nyingi jambo la hatari ulifanyapo kwa wakati husika, waweza kujuta baadaye.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 "eLimu | Msamiati: Nasaba/ Ukoo". learn.e-limu.org. Iliwekwa mnamo 2022-04-12.
  2. Ngii, Jacline (2010-12-13). "Majuto Ni Mjukuu". Kiswahili Story Database (0).