Michelangelo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Michelangelo Buonarroti
Sanamu ya Daudi
Picha ya Hukumu ya Mwisho kwenye ukuta wa Kikanisa cha Sistina (Vatikano)

Michelangelo di Lodovico Buonarroti Simoni (6 Machi 1475 - 18 Machi 1564) alikuwa msanii nchini Italia aliye maarufu kama mchongaji, mchoraji, msanifuujenzi na mshairi. Huhesabiwa kati ya wasanii muhimu zaidi wa zama ya mwamko.

Kati ya kazi zake maarufu zaidi ni sanamu ya kijana Daudi na michoro ya ukutani wa Kikanisa cha Sisto IV huko Vatikano mjini Roma alichopamba kwa hadithi na watu wa Biblia.

Kati ya kazi zake maarufu kama msanifuujenzi ni hasa kuba ya Basilika la Mt. Petro kwenye Vatikano mjini Roma.

Upande wa dini, alikuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki, tena mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Michelangelo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.