Kikanisa cha Sisto IV

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jengo la pembenne katikati ya picha ndilo Kikanisa cha Papa Sisto IV.
Mchoro wa ukutani wa Yesu kumpa Mt. Petro funguo za ufalme wa mbinguni, kazi ya Perugino.
Dari ya Kikanisa cha Sisto IV ilichorwa na Michelangelo.
Mchoro maarufu zaidi wa Michelangelo ni Mungu akimuumba Adamu.
Hukumu ya mwisho ilivyochorwa na Michelangelo katika ukuta juu ya altare.

Kikanisa cha Sisto IV (kwa Kiitalia Cappella Sistina) ni kikanisa kikubwa nchini Vatikani, ambayo ndiko anakoishi Papa wa Kanisa Katoliki lote duniani.

Kikanisa hicho kilijengwa miaka 1473-1481 na Giovanni dei Dolci kwa ajili ya Papa Sisto IV.

Kikanisa hicho kinatumika mara chache kwa ibada muhimu sana, na hasa kwa uchaguzi wa Papa mpya unaofanywa na makardinali wote wasiozidi umri wa miaka 80.

Kwa kawaida zaidi ni mahali pa utalii kutokana na sanaa zilizochorwa kutani na darini hasa na Michelangelo, mchoraji wa Renaissance miaka 1505-1541.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons