Nenda kwa yaliyomo

Kardinali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kadinali)
Mavazi maalumu ya kardinali ni ya rangi nyekundu kumaanisha uaminifu wake unaotakiwa kufikia hatua ya kuuawa (kumwagika damu). Hapa yameonyeshwa kwenye dirisha la duka la mavazi ya Kikanisa huko Roma, Italia.
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria

Muundo

Papa: Fransisko
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Liturujia ya Trento Milano Toledo Braga Lyon Canterbury)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Kardinali ni cheo kimojawapo cha juu katika Kanisa Katoliki, hasa Kanisa la Kilatini, lakini si daraja takatifu.

Wenye kumchagua Papa

[hariri | hariri chanzo]

Mkutano wa makardinali ndio humchagua Papa mpya ambaye ni mkuu wa Kanisa hilo ambalo ni madhehebu ya Ukristo makubwa kuliko jumla ya mengine yote duniani. Uchaguzi hutokea baada ya Papa aliyetangulia kufa au kung'atuka. Lakini kardinali aliyefikia umri wa miaka 80 hashiriki tena katika uchaguzi wa Papa.

Kati ya kifo cha Papa na uchaguzi wa mwandamizi wake ni mkutano wa makardinali unaoongoza Kanisa lote kwa muda.

Uteuzi wa kardinali

[hariri | hariri chanzo]

Kwa kawaida kardinali huteuliwa kati ya maaskofu, lakini kuna pia makasisi wachache wanaoteuliwa na Papa kuwa kardinali bila kupewa uaskofu.

Mwenye kuteua makardinali ni Papa peke yake, naye ana haki ya kumteua kardinali hata bila kutangaza jina lake. Kardinali ya aina hiyo huitwa kwa Kilatini "in pectore" (yaani "moyoni"). Hii inaweza kutokea hasa kama ni kardinali kutoka nchi pasipo uhuru wa dini au nchi ambayo haina uhusiano mzuri na Kanisa Katoliki.

Wajibu wa makardinali

[hariri | hariri chanzo]

Wajibu mkubwa ni kumchagua mwandamizi wa Papa, lakini pia ni kazi yao kumshauri katika kuongoza Kanisa lote.

Kwa kawaida viongozi wa idara kadhaa za Kanisa wanapewa kofia ya kardinali.

Pia kwa sababu hiyo kuna idadi ya makardinali wanaoishi Vatikani au katika mitaa mingine ya jiji la Roma.

Hata hivyo kwa sasa wengine wengi wanaishi katika nchi mbalimbali, wakiongoza majimbo. Hiyo haina maana kwamba wao ni wakuu wa maaskofu wenzao wa nchi hiyo au kwamba wana mamlaka yoyote juu ya Kanisa la nchi hizo.

Idadi ya makardinali

[hariri | hariri chanzo]

Hakuna idadi maalumu ya makardinali na mnamo 7 Novemba 2021 walifikuwa 215.

Papa Paulo VI aliunda utaratibu kuwa wasiwepo zaidi ya makardinali 120 wenye haki ya kupiga kura. Wale waliofikia umri wa miaka 80 hawashiriki tena katika uchaguzi wa Papa mpya. Lakini kardinali hajiuzulu wala kustaafu: anaendelea na cheo na pia na haki ya kushiriki katika mkutano wa makardinali hadi kifo.

Kwa sababu ya uhusiano wao na Kanisa la Roma, kimapokeo makardinali wengi ni Waitalia, hata Mapapa walikuwa Waitalia watupu kwa karne nne mfululizo hadi alipochaguliwa Papa Yohane Paulo II, Mpolandi.

Lakini asilimia ya makardinali Waitalia imepungua: kabla ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia zaidi ya nusu walikuwa Waitalia, siku hizi hawafikii asilimia 25.

Tarehe hiyo makardinali walikuwa wanatokea nchi 87 za mabara yote.

Kati yao wenye haki ya kupiga kura walikuwa 120 wakitokea nchi 65 tofauti.

Mgawanyo wa makardinali kwenye mabara ni kama ifuatavyo:

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]