Ekumeni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Neno ekumeni linamaanisha tapo la Ukristo linalolenga kurudisha umoja kamili kati ya madhehebu yake mbalimbali.

Msingi wake ni imani inayowaunganisha katika Yesu Kristo na kwa njia yake katika Utatu mtakatifu, yaani Mungu pekee aliye Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Neno linatokana na Kigiriki oikouméne, linalomaanisha kwa asili sehemu ya dunia iliyokaliwa na watu; hivyo likaja kuwa na maana ya jambo linalohusu waamini duniani kote.

Ekumeni ilianza kati ya Waprotestanti, hasa lilipofanyika Kongamano la Kimisionari la Kimtaifa huko Edimburg, mwaka 1910, ambapo waliohudhuria walisisitiza uhusiano kati ya umoja wa Wakristo na kazi ya uinjilishaji wa mataifa.

Mwaka 1937 iliundwa Halmashauri ya Kiekumeni ya Makanisa, ikijumlisha hata Waorthodoksi. Kwa sasa inawakilisha robo tu ya Wakristo wote.

Kanisa Katoliki liliingia kwa nguvu katika juhudi hizo kuanzia Papa Yohane XXIII (1958-1963) na Mtaguso wa pili wa Vatikano (1962-1965).