Ukristo katika karne za kwanza

Ukristo katika karne za kwanza ni sehemu ya historia ya Kanisa hadi mwaka 325 BK, ulipofanyika mtaguso mkuu wa kwanza huko Nisea, leo nchini Uturuki.
Kwa kawaida karne hizo tatu zinagawiwa pande mbili: wakati wa Mitume wa Yesu (hadi mwaka 100 hivi) na baada ya kifo chao wote.
Wakati wa Mitume
[hariri | hariri chanzo]Habari kuu za kipindi cha kwanza, kama ile ya siku ya Pentekoste Roho Mtakatifu kuwashukia wafuasi wa Yesu, zinapatikana hasa katika Matendo ya Mitume, kitabu kilichoandikwa na mwinjili Luka kwenye miaka ya 80. Humo unasimuliwa hasa uenezi wa Ukristo katika maeneo ya upande wa kaskazini wa Bahari ya Kati.
Tukio lingine muhimu linalosimuliwa na Luka ni uongofu wa Mtume Paulo, mwenezi mkuu wa Ukristo na mfafanuzi bora wa imani hiyo mpya.[1]
Pamoja na uenezi, linajitokeza badiliko kubwa la Wakristo: awali walikuwa wote Wayahudi ama kwa kuzaliwa ama kwa kuongoka,[2] nao wanaitwa Wakristo wa Kiyahudi. Lakini katika karne ya 1 tayari idadi yao ilizidiwa na ile ya Wakristo wa mataifa mengine.
Sambamba na hilo lugha ya kimataifa ya Kigiriki ilizidi kutumika badala ya Kiaramu, lugha mama ya Yesu na mitume wake.[3] Ndiyo sababu Agano Jipya limeandikwa lote kwa Kigiriki. Vitabu 27 vinavyoliunda vilianza kulinganishwa na vile vya Agano la Kale kama vitakatifu.
Tena Yerusalemu, uliokuwa mji mkuu wa Wayahudi na wa Wakristo wa kwanza, ulizidi kukosa umuhimu, hasa baada ya Mtume Petro na wenzake kuuhama au kuuawa. Wakati wa vita vya kwanza vya Kiyahudi hata waumini wa kawaida walihama, na waliporudi hakukuwa tena na hekalu, kwa kuwa lilibomolewa mwaka 70. Mbali ya hayo, uhusiano na Wayahudi ulizidi kuharibika, na hatimaye Wakristo walikatazwa wasishiriki tena ibada sinagogini.
Jumuia ya Roma, makao makuu ya dola, ilizidi kuwa muhimu, hasa baada ya kufikiwa na Petro na Paulo, ambao walimalizia huko kazi yao kwa kufia dini katika dhuluma ambayo ilianzishwa na Kaisari Nero mwaka 64 na kuendelea kwa kwikwi hadi mwaka 313.
Wakati wa watetezi wa imani
[hariri | hariri chanzo]Bila kujali dhuluma hiyo ya nyingine, Ukristo ulizidi kuenea ndani na nje ya Dola la Roma.
Ushujaa wa umati wa wafiadini na upendo kati ya Wakristo vinafikiriwa kuwa sababu kuu ya uenezi. Kutoka kwenye miji, imani ilizidi kuenea vijijini pia.
Pamoja na hayo, walianza kujitokeza waandishi mbalimbali kutetea Kanisa mbele ya serikali, na wengine kuchambua imani dhidi ya uzushi uliozidi kupata nguvu hasa kwa namna ya Gnosis. Waandishi hao ni kati ya wale wanaoitwa mababu wa Kanisa au walau waandishi wa Kikanisa.
Wakati huohuo matumizi ya vitabu vya Agano Jipya katika ibada yalizidi kujadiliwa na kutungiwa orodha rasmi (Kanuni ya Biblia).
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Oxford Dictionary of the Christian Church ed. F.L. Lucas (Oxford) entry on Paul
- ↑ Catholic Encyclopedia: Proselyte: "The English term "proselyte" occurs only in the New Testament where it signifies a convert to the Jewish religion (Matthew 23:15; Acts 2:11; Acts 6:5; etc.), though the same Greek word is commonly used in the Septuagint to designate a foreign sojourner in Palestine. Thus the term seems to have passed from an original local and chiefly political sense, in which it was used as early as 300 B.C., to a technical and religious meaning in the Judaism of the New Testament epoch."
- ↑ Ehrman, Bart D. (2012). Did Jesus Exist?: The Historical Argument for Jesus of Nazareth. HarperCollins, pp 87- 90.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Vidmar, John (2005). The Catholic Church Through the Ages: A History (kwa Kiingereza) (tol. la Illustrated, annotated). Paulist Press. ISBN 978-0-8091-4234-7.
- Bond, Helen K. (2012). The Historical Jesus: A Guide for the Perplexed. Bloomsbury Academic. ISBN 978-0-567-12510-1.
- Chadwick, Henry (1993). The Early Church. The Penguin History of the Church. Juz. la 1 (tol. la revised). Penguin Books. ISBN 978-0-14-023199-1.
- Dunn, James D.G. Jews and Christians: The Parting of the Ways, AD 70 to 135. pp 33–34. Wm. B. Eerdmans Publishing (1999). ISBN 978-0-8028-4498-9.
- Fredriksen, Paula (1999). Jesus of Nazareth, King of the Jews: A Jewish Life and the Emergence of Christianity. Vintage Books. ISBN 978-0-679-76746-6.
- Freeman, Charles (2011). A New History of Early Christianity. Yale University Press. ISBN 978-0-300-17083-2.
- González, Justo L. (1987). A History of Christian Thought. Juz. la 1: From the Beginnings to the Council of Chalcedon (tol. la revised). Abingdon Press. ISBN 978-0-687-17182-8.
- González, Justo L. (2010). The Story of Christianity. Juz. la 1 The Early Church to the Dawn of the Reformation (tol. la revised and updated). HarperCollins. ISBN 978-0-06-185588-7.
- Hopkins, Keith (1998). "Christian Number and Its Implications". Journal of Early Christian Studies. 6 (2). Johns Hopkins University Press: 185–226. doi:10.1353/earl.1998.0035. ISSN 1086-3184. S2CID 170769034. Kigezo:Project MUSE.
- Klutz, Todd (2000). "Paul and the Development of Gentile Christianity". Katika Esler, Philip F. (mhr.). The Early Christian World. Routledge Worlds. Routledge. ku. 178–190. ISBN 978-1-032-19934-4.
- MacCulloch, Diarmaid (2010). Christianity: The First Three Thousand Years. Penguin Books. ISBN 978-1-101-18999-3.
- Marcus, Joel (2006). "Jewish Christianity". Katika Mitchell, Margaret M.; Young, Frances M. (whr.). The Cambridge History of Christianity. Juz. la 1: Origins to Constantine. Cambridge University Press. ku. 87–102. doi:10.1017/CHOL9780521812399. ISBN 978-1-139-05483-6.
- McGrath, Alister (2013). Christian History: An Introduction. Wiley-Blackwell. ISBN 978-1-118-33780-6.
- Mitchell, Margaret M. (2006). "Gentile Christianity". Katika Mitchell, Margaret M.; Young, Frances M. (whr.). The Cambridge History of Christianity. Juz. la 1: Origins to Constantine. Cambridge University Press. ku. 103–124. doi:10.1017/CHOL9780521812399. ISBN 978-1-139-05483-6.
- Schnelle, Udo (2020). The First One Hundred Years of Christianity: An Introduction to Its History, Literature, and Development. Ilitafsiriwa na Thompson, James W. Grand Rapids, Michigan: Baker Academic. ISBN 978-1-4934-2242-5.
- Seifrid, Mark A. (1992). Justification by Faith: The Origin and Development of a Central Pauline Theme. Novum Testamentum, Supplements. Leiden: Brill Publishers. ISBN 978-90-04-09521-2. ISSN 0167-9732.
- Wilken, Robert Louis (2012). The First Thousand Years: A Global History of Christianity. Yale University Press. ISBN 978-0-300-11884-1.
Marejeo mengine
[hariri | hariri chanzo]- Pelikan, Jaroslav Jan (1975). The Christian Tradition: The Emergence of the Catholic Tradition (100–600). Chicago: University of Chicago Press. ISBN 978-0-226-65371-6.
- Stark, Rodney (1997). The Rise of Christianity. New York: HarperCollins. ISBN 978-0-06-067701-5.
- Taylor, Joan E. (1993). Christians and the Holy Places: The Myth of Jewish-Christian Origins. Oxford: Oxford University Press. ISBN 978-0-19-814785-5.
- Thiede, Carsten Peter (2003). The Dead Sea Scrolls and the Jewish Origins of Christianity. Basingstoke: Palgrave Macmillan. ISBN 978-1-4039-6143-3.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Early Christian Sources English translations of the surviving writings of the early Christians.
- Early Christians (archived 1 September 2014)
- PBS Frontline: The First Christians
- First Christians and Rome
- Cave in Jordan Said to Have Been Used by Early Christians Biblical Archaeology Review (archived 7 January 2010)
| Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ukristo katika karne za kwanza kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |