Dominiko wa Guzman

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Dominiko Guzman)
Dominiko wa Guzmán, mwanzilishi wa Shirika la Ndugu Wahubiri

Dominiko wa Guzmán (Calaroga (Hispania) 1170 hivi - Bologna (Italia) 6 Agosti 1221) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki akaanzisha Shirika la Wahubiri.

Alitangazwa mtakatifu na Papa Gregori IX tarehe 2 Julai 1234.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Agosti[1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Dominiko wa Guzman alikuwa mkanoni wa jimbo la Burgo de Osma-Ciudad de Osma: mwaka 1203 aliongozana na askofu wake Diego wa Acevedo katika safari ya kibalozi kwa niaba ya mfalme Alfonso VIII wa Castilia kwa mfalme Valdemaro II wa Denmark. Wakati wa kurudi, wakipitia mkoa wa Langadoque (Ufaransa Kusini), waling'amua uzushi wa Wakatari ulivyoenea naye akaamua kuungana na mabalozi wa Papa Inosenti III katika jitihada za kurudisha watu hao katika Kanisa Katoliki.

Akikusanya kundi dogo la wasichana walioacha Ukatari, maka 1207 alianzisha huko Notre-Dame-de-Prouille, karibu Fanjeaux, monasteri ya kike ambayo ikawa kitovu cha kazi yake ya kitume.

Dominiko aliendelea kuwahubiri kwa amani Wakatari hata baada ya balozi wa Papa Petro wa Castelnau kuuawa (1208), akikataa kujiunga na vita vya msalaba vilivyotangazwa dhidi ya Wakatari.

Kwa msaada wa askofu wa Tolosa Folco, mwaka 1215 alikusanya wenzi kadhaa wenye nya ya kuhubiri kama yeye akawaingiza katika maisha ya kitawa: shirika hilo lilipata kwanza kibali fulani cha Papa Inosenti III halafu kibali rasmi cha mwandamizi wake, Papa Onori III, tarehe 22 Desemba 1216.

Baada ya hapo Shirika la Ndugu Wahubiri lilienea kati Ulaya nzima, hasa katika miji ambapo vilikuwa vinaanza vyuo vikuu, kama vile vya Bologna na Paris, vilivyosaidiwa sana na Wadominiko kupata ustawi.

Kwa agizo la Mtaguso IV wa Laterano ndugu hao walipaswa kujichagulia kanuni iliyowahi kukubaliwa na Kanisa, wakaamua kushika ile ya Agostino wa Hippo, wakiiongezea katiba ya kwao, maarufu hasa kwa kutumia kiasi fulani cha demokrasia, ambayo ilitumiwa kama mwongozo kwa nyingine hata za kiserikali.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.