Mtawa
(Elekezwa kutoka Utawa)
Jump to navigation
Jump to search
Mtawa ni mtu anayejitenga na ulimwengu ili kuishi maisha maadilifu.
Katika dini mbalimbali, mfano mmojawapo wa utawa ni ule wa wamonaki. Lakini katika Ukristo, hasa wa Magharibi historia ya Utawa ilitokeza aina nyingine mbalimbali.
Katika Kanisa Katoliki, ni mwamini yeyote aliyejiweka wakfu kwa Mungu hasa kwa kushika useja mtakatifu, lakini kwa kawaida pia ufukara na utiifu.
Mara nyingi watawa wanaunda mashirika yenye karama moja inayofafanuliwa na kuratibiwa katika kanuni na katiba maalumu.
Mtawa anaweza kuwa mwanamume au mwanamke, mwenye daraja takatifu au la.
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtawa kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |