Nadhiri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Samsoni alikuwa mnadhiri tangu tumboni mwa mama yake.
Sista Mbenedikto akiweka nadhiri ya daima na kuwekwa wakfu kama bikira (2006).
Ibada ya kuweka nadhiri katika monasteri ya maisha ya ndani tu.

Nadhiri (kwa Kiebrania נדר, neder) ni ahadi inayotolewa kwa Mungu, kama k.mf. Biblia inavyoonyesha (Law 27; Amu 11; Mdo 21:23; 23:21).

Yeyote anaweza kuweka nadhiri anavyopenda, lakini kuna nadhiri zilizoratibiwa na sheria, hasa sheria za Kanisa, kama zile za kitawa.

Katika mashirika mengi, zinahesabiwa tatu ambazo zinaendana: useja mtakatifu, ufukara na utiifu.

Baadhi yanaongeza nyingine (nadhiri ya nne), k.mf. kujitoa hadi kufa kwa ajili ya Wakristo walio katika hatari ya kupoteza imani (kwa Wamersedari), kutekeleza toba ya kudumu kwa Waminimi, utiifu kwa Papa kwa Wajesuiti, na utumishi wa walio fukara zaidi kwa wafuasi wa Mama Teresa wa Kolkata.

Nadhiri zinaweza kuwa za muda au za daima. Mara nyingi zile za muda zinatangulia na kuandaa zile za daima.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.