Kiburi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kiburi kadiri ya Adolfo Wildt (1868-1931) katika Chuo kikuu cha serikali huko Milano (Italia).
Kiburi kilivyochongwa katika kinara cha 10 cha Palazzo Ducale huko Venezia (Italia).
Kiburi kilivyochorwa katika kanisa kuu la Chartres (Ufaransa).

Kiburi ni hamu isiyoratibiwa ya kujipatia ukuu dhidi ya wengine, pengine hata dhidi ya Mwenyezi Mungu. Kiburi ni hisia na fikra zilizopotoka kuhusu ukweli na uhalisia wa mambo. Lusifa anatajwa kuwa na fikra za kuwa juu ya Mungu, hakika huo ni upotofu wa hali ya juu sana kwa kuwa haiwezekani kwa namna yoyote kuwa zaidi ya Mungu hata kwa mfumbo wa jicho moja. Ni sawa na kusema mtoto amzae baba au mama yake. Haiwezekani chombo cha udongo kikawa na uwezo zaidi ya mfinyanzi kwa kuwa ni kizuri na kinavutia na kusifiwa na watu wengi, huku aliyekifinyanga hajulikani[1]. Isaya 29:16 kinasema, "Ninyi mnapindua mambo; Je! Mfinyanzi ahesabiwe kuwa kama udongo; kitu kilichofinyangwa kimnene yeye aliyekifinyanga, 'Hakuna mfinyanga huyu'; au kitu kilichoumbwa kimnene yeye aliyekiumba, 'Yeye hana ufahamu'?"

Katika Ukristo ndicho kilema kikuu cha roho ya shetani na binadamu aliyepotoka.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. James Mwalubalile, Nguvu ya Kiburi (Dhambi Mama), 2021.