Kujiamini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kujiamini (en:confidence) ni hisia ya kuwa hakika na ama kuwa nadharia tete ama matarajio ni ya kweli ama kuwa njia ambayoimechaguliwa ni zuri zaidi ama ina mafanikio. Kujiamini ni kuwa na uhakika wa binafsi. Ubarakala ama kiburi katika ulinganisho huu ni kujiamini kusikokuwa na msingi na kuamini mtu ama kitu kuwa na uwezo ama kweli wakati sivyo. Kujiamini mno au kiburi ni kuwa na imani kupita kiasi, katika mtu ama kitu bila ya kufikiria kwamba kuna uwezekano wa kutofaulu. Kisayansi, hali fulani inaweza kuamuliwa baada ya matokeo kuwa yamepatikana au la. Kujiamini kunaweza kumaanisha utabiri wa kujitimizia kwa kuwa wale wasiokuwa nao wanaweza kukosa kufaulu au washindwe kujaribu kwa kuwa hawajiamini, na wale wenye kujiamini wanaweza kufaulu kwa sababu wanajiamini badala ya uwezo wao.

Kujiamini[hariri | hariri chanzo]

Kujiamini haimaanishi lazima kuwa ni 'mtu binafsi kuwa na imani kumhusu' ama imani ya uwezo wa mtu kufanikiwa. Kwa mfano, mtu anaweza kukosa kuwa stadi katika mchezo au shughuli fulani, lakini bado 'awe na imani' katika mazoea ya mtu, kwa sababu hasisitizi matokeo ya shughuli hiyo. Kwa hivyo, sifa kuu ya kujiamini, ni kukubali matokeo mbalimbali ya hali fulani, yawe mazuri ama mabaya. Iwapo mtu hataegemea kwa matokeo mabaya tu anaweza 'kujiamini mno' kwa sababu hafikirii zaidi kuhusu kushindwa au (usahihi zaidi) ya kukemewa na wenzake iwapo atashindwa. Hivyo basi mtu anaweza kuzingatia zaidi hali halisi ambayo ina maana kuwa kuna matarajio makubwa ya kufurahia na kufaulu katika hali hiyo. Iwapo kuna kipengele cha 'kujiamini' kimsingi huu ni uwezo wa mtu kuvumilia matokeo yoyote yale; uhakika kwamba mtu anweza kukabiliana na hali bila kujali kitakachotokea. Mtu kujiamini katika uwezo wake wa kufanya shughuli fulani kutokana na tajiriba ya awali iliyofaulu inaweza kuongezea,kuchangia dhana ya Kujiamini.

Kwa jumla wakati mtu ana mwelekeo wa kutojali kuhusu maisha pia wanaweza kuonekana kuwa wanaojiamini wakati hili hata hili si la muhimu. Badala yake ni uwezekano kwamba mtu huyo hana uwezo mzuri wa kuvumilia na hatathmini athari za hali fulani vizuri na mara nyingi hisia za wengine. Kwa sababu hii wanawezakuwa na ubarakala kwa sababu wanaweza kuonyesha hali ya ushindi na wakose kujali maslahi ya wengine wanapotathmini matokeo na hisia za wengine kuwa zisizo na umuhimu badala ya za kukubalika. Kadri muelekeo huu unavyojidhihirisha ndivyo uwezekano wa saikopatholojia ulivyo mkubwa.

Kuamini wengine[hariri | hariri chanzo]

Watu wanaweza kuamini watu wengine au kuvutiwa nao namna ambayo inazidi uwezo wao. Kwa mfano, mtu anaweza kuamini polisi kuwa na uwezo wa kumlinda ama kuwa na imani kuwa timu fulani itashinda katika shindano fulani. Maneno imani na kujiamini ni visawe yanapotumika kwa maana hii.

Angalia Pia[hariri | hariri chanzo]