Sala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Yesu akisali katika mateso yake huko Gethsemane kadiri ya Heinrich Hofmann
Mwanamume Mshinto wa Japani akisali peke yake
Mikao muhimu ya salat katika baadhi ya madhehebu ya Uislamu
Wanawake Wakristo wa Urusi wakisali pamoja

Sala (kutoka neno la Kiarabu صلاة‎, ṣalāh, wingi wake ni صلوات, ṣalawāt, na maana yake ni "sala iliyoratibiwa", tofauti na "dua", "ombi") ni njia ambayo binadamu anauelekea ulimwengu wa roho, hasa kwa lengo la kuongea na Mungu kwa sauti au kimoyomoyo.

Malengo yake yanaweza kuwa tofauti: kusifu, kushukuru, kuomba au kujiachilia.

Upande wa pili sala ni kutafakari ili kusikiliza na kuelewa ujumbe wa Mungu.

Sala inaweza kufanywa na mtu peke yake au na wengi pamoja, hata kwa kuimba.

Dini zinaelekeza waumini wake kusali kwa namna mbalimbali.

  • Katika Uyahudi siku za kawaida kuna sala 3.
  • Katika Uislamu sala inatakiwa mara 5 kwa siku, ingawa zinahimizwa pia sala za hiari. Zulia inatumika kwa ajili ya kumsujudia Mungu.

External links[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sala kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.