Nenda kwa yaliyomo

Msamaha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Msamaha (kutoka neno la Kiarabu) ni uamuzi wa Mungu au mtu wa kutofuatilia makosa ambayo ametendewa.[1][2]

Ni kinyume kabisa cha kisasi lakini pia ni tofauti na kutetea, kusahau na kupatana. Kwa kawaida unaendana na ombi la mtu aliyekiri makosa.

Pengine neno msamaha linatumika kwa uamuzi wa rais au mtawala mwingine wa kutoa gerezani baadhi ya watu kabla adhabu yao haijakamilika, hasa katika nafasi ya kuingia madarakani au ya sikukuu nyingine. Vilevile kuhusu ondoleo la deni au wajibu mwingine.[3][4]

Elimunafsia inaonyesha kwamba utoaji wa msamaha unaleta nafuu kwa mtu anayeutoa, na nafuu hiyo inaweza kuenea kutoka nafsini hata mwilini,[5][1][6][7]

Dini nyingi zinasisitiza umuhimu wa kusamehe wengine kuhusiana na haja ya kusamehewa nao lakini pia na Mungu kutokana na ukosefu unaomuathiri kila binadamu.

  1. 1.0 1.1 "American Psychological Association. Forgiveness: A Sampling of Research Results." (PDF). 2006. Iliwekwa mnamo 2009-02-07.
  2. What Is Forgiveness? The Greater Good Science Center, University of California, Berkeley
  3. DEBT FORGIVENESS Ilihifadhiwa 31 Oktoba 2013 kwenye Wayback Machine. OECD, Glossary of Statistical Terms (2001)
  4. Loan Forgiveness Ilihifadhiwa 13 Novemba 2013 kwenye Wayback Machine. Glossary, US Department of Education
  5. Graham, Michael C. (2014). Facts of Life: ten issues of contentment. Outskirts Press. uk. 268. ISBN 978-1-4787-2259-5.
  6. What Is Forgiveness? The Greater Good Science Center, University of California, Berkeley
  7. "Forgiving (Campaign for Forgiveness Research)". 2006. Iliwekwa mnamo 2006-06-19.