Rais

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Rais (kutoka kar.:رئیس) ni cheo cha mkuu wa nchi katika serikali ya jamhuri. Rais huwa anachaguliwa ama na wananchi wote au na bunge.

Kuna aina mbili za rais kufuatana na katiba za nchi mbalimbali:

Katika muundo wa serikali ya kibunge shughuli za serikali zinasimamiwa na waziri mkuu. Madaraka ya rais katika muundo huo hufanana na madaraka ya mfalme wa kikatiba isipokuwa hayupo kama rais kwa muda wa maisha yake kama mfalme.

Katika Uswisi kazi ya rais hazitekelezwi na mtu mmoja bali na Halmashauri ya Shirikisho kwa ujumla.