Kamati

Kamati (kutoka neno la Kiingereza "committee") ni kundi la watu walioteuliwa au kuchaguliwa kwa ajili ya kazi maalum.[1][2][3]
Mara nyingi huteuliwa miongoni mwa wajumbe wa kikundi au kundi kubwa na wakati mwingine hutarajiwa pia kufanya utafiti wa kina kuhusu jambo maalum kwa muda fulani na hatimaye kutoa mapendekezo kulingana na matokeo ya utafiti wao.[4] Kwa mfano nchini Tanzania Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imeundwa chini ya Kanuni ya 118 (1) & (2) ikisomwa pamoja na fasili ya 1(c) ya Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016. Kwa mujibu wa fasili ya 4 (1) ya Nyongeza ya Nane, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imepewa majukumu yafuatayo: (a) Kuchunguza na kutoa mapendekezo kuhusu masuala yote ya haki, kinga na madaraka ya Bunge yatakayopelekwa na Spika; (b) Kushughulikia mambo yanayohusu maadili ya Wabunge yatakayopelekwa na Spika.[5]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Roberts, A., & Smith, J. (2014). *Committees and Organizational Management*. Routledge. Kitabu kinachofafanua aina, majukumu, na utendaji wa kamati katika mashirika mbalimbali.
- ↑ Fowler, A. (2016). "Parliamentary Committees: Functions and Effectiveness". *Journal of Legislative Studies*, 22(3), 345–362. Makala ya kisayansi kuhusu kamati za bunge na mchango wake katika uendeshaji wa serikali.
- ↑ United Nations. (2018). "Committee Structures and Governance". *UN Guidelines on Organizational Structures*. https://www.un.org/en/committees-governance. Mwongozo wa kimataifa kuhusu jinsi kamati zinavyoundwa na kazi zao.
- ↑ Kothari, C. R. (2019). *Research Methodology: Methods and Techniques*. New Age International. Kitabu kinachofafanua jinsi kamati zinavyotumika katika utafiti wa kijamii na usimamizi wa miradi.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2020-09-30. Iliwekwa mnamo 2020-08-06.
| Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kamati kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |