Bunge
Bunge ni chombo cha kutunga sheria na pia ni mmoja wa mihimili mitatu inayounda mfumo wa utawala kulingana na mgawanyo wa madaraka katika dola. Mihimili mingine ni mahakama na serikali.
Bunge ni chombo kinachotokana na mfumo wa utawala wa Westminster, ambao umerithiwa na nchi nyingi duniani kutoka Uingereza. Kutokana na mfumo huo kuenea, mara nyingi Bunge la Uingereza huitwa "Mama wa Bunge" duniani.
Bunge la kwanza nchini Uingereza liliundwa wakati wa utawala wa Mfalme Henri III katika karne ya 13. Bunge hilo lina sehemu mbili, Bunge la Makabwela na Bunge la Mabwanyeye.
Katika nchi nyingi zinazofuata mfumo wa Westminster, Waziri Mkuu huwa ndio kiongozi mkuu wa serikali bungeni.
Shughuli za bunge husimamiwa na mbunge aliyechaguliwa kama mwenyekiti, rais au spika wa bunge.
Kuna aina mbili za bunge:
- Bunge la "chumba kimoja" ambako wawakilishi wote wa wananchi hukaa na kufanya maazimio pamoja
- Bunge la "vyumba viwili" ambako kitengo kikubwa zaidi kina kazi ya kutunga sheria na wabunge wake huchaguliwa moja kwa moja na wananchi katika majimbo ya uchaguzi yanayotakiwa kuwa takriban na idadi ya wapiga kura sawa. Kitengo kingine mara nyingi huitwa "senati" au "chumba cha juu" kwa kawaida ni kidogo zaidi, wabunge wake huchaguliwa ama na wawakilishi wa mikoa au majimbo au wanateuliwa pia kufuatana na kanuni za katiba (k.m. kwa shabaha ya kuwakilisha makundi maalumu katika jamii) na madaraka yake kwa kawaida ni madogo lakini inathibitisha au kukataa sheria zilizoamuliwa na bunge la kwanza; lakini hapa kuna tofauti nyingi kati ya nchi na nchi.[1]
Mabunge ya Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Orodha ya Wabunge wa Tanzania
Ona pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Kamusibunge kamusi bunge.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- (Kiingereza) Bunge la Tanzania Archived 19 Novemba 2007 at the Wayback Machine.
- (Kiingereza) Bunge la Afrika Kusini
- Bunge la Umoja wa Afrika Archived 15 Juni 2006 at the Wayback Machine.
- (Kiingereza) Bunge la Ghana
- (Kiingereza) Bunge la Uingereza Archived 23 Februari 2011 at the Wayback Machine.
- (Kiingereza) Bunge la Ulaya Archived 27 Novemba 2005 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |