Ufalme wa Muungano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ufalme wa Muungano wa Britania
na Eire ya Kaskazini

United Kingdom of Great Britain
and Northern Ireland
Bendera ya Ufalme wa Muungano Nembo ya Ufalme wa Muungano
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: "Dieu et mon droit" (Kifaransa)
"Mungu na haki yangu"
Wimbo wa taifa:

"God Save the Queen"
Lokeshen ya Ufalme wa Muungano
Mji mkuu London
51°30′ N 0°7′ W
Mji mkubwa nchini London
Lugha rasmi Kiingereza
Serikali
Waziri Mkuu wa Ufalme wa Muungano
Unitary, Katiba kifalme
Theresa May MP
'
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
243,610 km² (80th)
1.34%
Idadi ya watu
 - 2013 kadirio
 - 2011 sensa
 - Msongamano wa watu
 
64,100,000 (22nd)
63,181,775
255.6/km² (51st)
Fedha Pound Sterling (£) (GDP)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
Greenwich Mean Time (GMT) (UTC+0)
British Summer Time (BST) (UTC+1)
Intaneti TLD .uk
Kodi ya simu +44

-Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini (kwa Kiingereza: United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland); kifupi "Ufalme wa Muungano" (Kiing.: United Kingdom) ni nchi ya visiwani ya Ulaya ya kaskazini-magharibi.

Mara nyingi huitwa kwa Kiswahili "Uingereza" tu ingawa nchi ya Uingereza ni moja tu kati ya sehemu za ufalme huo pamoja na Uskoti, Welisi na Eire ya Kaskazini.

Nchi iliongoza mapinduzi ya viwanda duniani, ilienea katika mabara yote kwa makoloni yake mengi ikabaki hadi leo kati ya nchi muhimu zaidi ulimwenguni.

Ni mwanachama mwanzilishi wa Umoja wa Mataifa, ambapo ana kiti cha kudumu na kura ya turufu katika Halmashauri ya Usalama, pia ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya, ingawa inajiandaa kujitoa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Milki kubwa kwenye kisiwa cha Britania Kuu ilikuwa Uingereza. Tangu mwaka 1284 Welisi ilitawaliwa na Uingereza na katika Sheria ya Muungano (Act of Union) ya 1536 ilikuwa sehemu ya Milki ya Uingereza. Sheria ya Muungano ya 1707 iliunganisha milki mbili za Uingereza na Uskoti kuwa Milki ya Britania Kuu. Nchi zote mbili ziliwahi kuwa chini ya mfalme mmoja tangu mwaka 1603. Tangu wakati uleule Ufalme wa Eire (Ireland) ilitawaliwa na Uingereza pia. Sheria ya 1800 iliunganisha Ufalme wa Britania Kuu na Ufalme wa Eire na hivyo kuunda Ufalme wa Maungano (United Kingdom of Great Britan and Ireland).

Baada ya Vita ya uhuru ya Eire bunge la London kwa sheria ya 1920 (Government of Ireland Act 1920) liligawa Ireland kwa sehemu mbili za Northern Eireland na Southern Ireland. Wabunge waliochaguliwa katika Ireland ya Kusini walijitangaza kuwa bunge la Eire na kwa mapatano ya 1922 uhuru wa Dola Huru la Eire ilitambuliwa. Nchi mpya ilijiita tangu 1922 1937 "Jamhuri ya Eire na kuendelea kama nchi ya pekee. Mikoa ya Northern Ireland iliendelea kuwa sehemu za Ufalme wa Maungano.

Elderly lady with a yellow hat and grey hair is smiling in outdoor setting.
Elizabeth II, Malkia wa Ufalme wa Muungano na wa nchi mbalimbali za Commonwealth.

Mwaka 1999 Uskoti, Welisi na Northern Ireland zilirudishwa bunge zao za pekee.

Uskoti ilikuwa na harakati pana ya kuondoka katika Ufalme wa Maungano lakini katika kura ya watu wa Uskoti ya mwaka 2014 asilimia 55 waliamua kubaki.

Kumbe kura ya wananchi wa Ufalme mzima ya mwaka 2016 iliamua kuondoka katika Umoja wa Ulaya kwa asilimia 51.9.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Upande wa dini, kadiri ya sensa ya mwaka 2011, 59.5% za wakazi ni Wakristo (hasa wa Anglikana, halafu Wakatoliki, Wakalvini na wengineo), 4.4% ni Waislamu, 1.3% ni Mabanyani. 25.7% hawana dini yoyote.

Muungano na utawala[hariri | hariri chanzo]

Bendera Nchi Hali Wakazi Vitengo Mji mkuu
Flag of England.svg
Uingereza Ufalme 50,431,700

Mikoa
Wilaya

London
Flag of Scotland.svg
Uskoti Ufalme 5,094,800

Wilaya

Edinburgh
Flag of Wales 2.svg
Welisi Utemi 2,958,600

Wilaya

Cardiff
Hapana Eire ya Kaskazini Jimbo 1,724,400

Wilaya

Belfast

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Serikali
Taarifa za jumla
Safari

Anwani ya kijiografia: 55°N 3°W / 55°N 3°W / 55; -3

Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Denmark | Estonia | Hispania | Hungaria | Ireland | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Ufalme wa Muungano | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ufalme wa Muungano kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.