Kifupi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kifupisho au Kifupi ni njia ya kutaja au kuandika neno kwa namna fupi kuliko kawaida.

Watu hutumia kifupi mara nyingi wakiandika neno au kundi la maneno fulani mara nyingi. Hasa pale ambako nafasi ya kuandika ni ndogo mafupisho ya aina hii yako kawaida kama vile kwenye SMS, kamusi au maorodhesho ya vitu.

Vifupisho vimekuwa pia kawaida kutaja vitengo vya serikali kama "JKT" (jeshi la kujenga taifa), makampuni kama "SMP" (Southern Paper Mills") au vyama vya kisiasa kama "CCM" (chama cha mapinduzi).

Vifupisho vya pekee huitwa pia akronimi ni maneno ambayo yameunganishwa kwa herufi za kwanza za maneno mengine. Mifano yake ni UKIMWI (=Uhaba wa KInga MWIlini) au Laser (= Laser - Light Amplification through Stimulated Electron Radiation).


Vifupisho katika kamusi[hariri | hariri chanzo]

Kamusi ya KKS inatumia vifupi vifuatavyo:

 • agh. - aghlabu
 • ele - elekezi
 • fiz - fizikia
 • kb - kibaaria
 • kd - kidini
 • kem - kemia
 • kh - kihusishi
 • ki - kiingizi
 • kl - kielezi
 • k.m. - kwa mfano
 • kt - kitenzi
 • ku - kiunganishi
 • k.v. - kama vile
 • ksh - kishairi
 • kv - kivumishi
 • kw - kiwakilishi
 • kz - kizamani
 • ms - msemo
 • mt - methali
 • nh - nahau
 • n.k. - na kadhalika
 • nm - nomino
 • sie - sielekezi
 • taz. - tazama

Vifupi vya Kisiasa na kiserikali[hariri | hariri chanzo]

Vifupisho vintaumiwa mara nyingi kwa kubadilisha maana asilia kwa kusidi la kutania au kufanya jambo linalijadiliwa kuonekana kama kichekesho.

Mifano yake ni tafsiri ya FFU (kikosi cha polisi ya Tanzania cha kukandamiza ghasia) kama "Fanya Fujo Uone" au ya CCM (chama tawala cha miaka mingi ncini Tanzania) kama "Chukua Chako Mapema".Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

 • Acronym Finder - largest acronym site with many ways to search for acronyms and abbreviations in many languages. Over 10 year history.
 • All Acronyms - a website with a large number of abbreviations and acronyms