Chama cha Mapinduzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Chama cha Mapinduzi (CCM) ni chama tawala nchini Tanzania. CCM ilizaliwa 5 Februari 1977 baada ya kuungana kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa kikitawala Tanzania Bara na Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa chama tawala cha Zanzibar wakati huo. Chama cha Mapinduzi kilikuwa kikiongozwa na Mwalimu Nyerere na Afro-Shiraz Party kilikuwa chini ya Amaan Karume.

Itikadi[hariri | hariri chanzo]

CCM kina wafuasi wengi vijijini.

Kwa miaka mingi CCM ilikuwa ikifuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Itikadi hii ilipewa nguvu za kisera mwaka 1967 lilipotangazwa Azimio la Arusha. Kutokana na azimio hilo uchumi uliwekwa mikononi mwa umma. Itikadi hii pia ilisisitiza umuhimu wa kuishi pamoja hasa katika vijiji vya Ujamaa.

Uchaguzi[hariri | hariri chanzo]

CCM imekuwa ikishinda chaguzi za Urais toka mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa nchini Tanzania. Chama hicho kimekuwa pia kikipata idadi kubwa ya wabunge wa Bunge la Muungano na Baraza la Wawakilishi. Chaguzi za vyama vingi Tanzania baada ya kurejeshwa kwa mfumo huo zilifanyika mwaka 1995, 2000, na 2005.

Uongozi[hariri | hariri chanzo]

Katika historia ya CCM kumekuwa na wenyeviti wanne:

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]