Serikali ya kibunge

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Serikali ya kibunge ni muundo wa siasa ambako serikali inategemea bunge. Ni tofauti na serikali ya kiraisi au aina kadhaa za ufalme ambako ama rais aliyechaguliwa au mfalme ana madaraka na mamlaka yasiyotegemea wabunge na wabunge hawana uwezo wa kumwondoa kiongozi huyu wakitaka. Isipokuwa kupitia masharti magumu.

Kuchaguliwa na bunge[hariri | hariri chanzo]

Kiongozi wa serikali huchaguliwa na bunge yaani idadi kuwba ya wabunge wanapaswa kumwunga mkono na kumpa kura. Kuna nchi ambako hata serikali yote huchaguliwa hivyo na bunge.

Kupinduliwa na bunge[hariri | hariri chanzo]

Bunge ina pia madaraka ya kumwondoa kwa njia zinazoelezwa katika katiba ya nchi. Njia za kumwondoa kiongozi wa serikali pamoja na mawaziri wake ni kutamka ya kwamba bunge halina imani tena naye. Tamko hili lamlazimishha kiongozi katika nchi nyingi kujiuzulu. Au rais anatakiwa kumtafuta kiongozi mpya atakayekubaliwa na wabunge wengi.

Nchi kadhaa zimefuata utaratibu wa kumpindua kiongozi wa serikali kwa tenda la kumchagua kiongozi mpya. Hapa hakuna nafasi ya kufukuza serikali bila kujua awali nani atakayeendelea.

Rais[hariri | hariri chanzo]

Nafasi ya rais katika nchi zinazofuata serikali ya kibunge ni zaidi ya heshima. Hana madaraka ya utendaji kwa sababu haya yamo mkononi mwa waziri mkuu anayechaguliwa na bunge. Nafasi kubwa wa rais au pia mfalme katika muundo wa kibunge ni wakati ambako serikali imepinduliwa au hakuna kikundi kimoja kikubwa kwa sababu hapo ndiye ais au mfalme atakayemteua mgombea wa waziri mkuu kwa kupelka jina lake bungeni.