Azerbaijan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Azərbaycan Respublikası
Jamhuri ya Azerbaijan
Bendera ya Azerbaijan Nembo ya Azerbaijan
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa:
Wimbo wa taifa: Azərbaycan Respublikasının Dövlət Himni
Lokeshen ya Azerbaijan
Mji mkuu Baku
40°22′ N 49°53′ E
Mji mkubwa nchini Baku
Lugha rasmi Kiazeri
Serikali Jamhuri
Ilham Aliyev
Artur Rasizade
Uhuru
Ilitangazwa
Ilikamilishwa

30 Agosti 1991
25 Desemba 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
86,600 km² (ya 114)
--
Idadi ya watu
 - 2014 kadirio
 - 1999 sensa
 - Msongamano wa watu
 
9 494 600[1] (ya 89)
7,953,438
105.8/km² (ya 100)
Fedha Manat (AZN)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+4)
(UTC+5)
Intaneti TLD .az
Kodi ya simu +994

-


Ramani ya Azerbaijan

Azerbaijan (pia: Azabajani, Azebajani) ni nchi ya Kaukazi kati ya Ulaya na Asia. Imepakana na bahari ya Kaspi, Urusi, Georgia, Armenia na Uajemi.

Azerbaijan ni pia jina la mikoa miwili katika Uajemi wa magharibi (Azerbaijan ya Mashariki na Azerbaijan ya Magharibi); nchini Uajemi takriban robo ya wakazi ni Waazeri; kwa jumla Waazeri katika Uajemi ni wengi kushinda walioko Azerbaijan yenyewe.

Eneo la Nakhichevan ni sehemu ya Azerbaijan ndani ya Armenia inayopakana na Uturuki na Uajemi.

Eneo la Nagorno-Karabakh ndani ya Azerbaijan linalokaliwa na Waarmenia lilijitangaza nchi huru mwaka 1991 lakini haijatambuliwa na umma wa kimataifa.

Azerbaijan ni nchi mwanachama wa baraza la Ulaya tangu 2001. Hivyo kisiasa inahesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya, lakini kijiografia mara nyingi yahesabiwa kuwa sehemu ya Asia ya Magharibi.

Azerbaijan ina historia ndefu lakini siku hizi inakaliwa hasa na Waazeri wanaoongea Kiazeri ambacho ni karibu sana na Kituruki na wengi wao (95%) ni Waislamu, hasa wa madhehebu ya Shia (85%). Wakristo ni 3.1%.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Mlima mkubwa ni Bazardüzü kwenye Kaukazi wenye kimo cha mita 4.466.

Ziwa kubwa ni Sarisu lenye eneo la km² 67.

Mto Kura unapita eneo la nchi na kuishia katika Bahari ya Kaspi baada ya mwendo wa km 1,515.

Azerbaijan ina visiwa viwili vya Pirallahı na Cilov kwenye Bahari ya Kaspi.

Kwenye rasi ya Abşeron kuna mafuta ya petroli.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Azerbaijan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Azerbaijan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.