Uzoroastro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Uzoroastro ni dini na falsafa inayopata jina lake kutoka nabii wake Zoroaster au Zarathustra, ambayo iliathiri imani ya Uyahudi na ya dini zilizotokana na Uyahudi.

Wazoroastro wanaamini katika ulimwengu na Mungu apitaye fikira, Ahura Mazda, ambaye ibada zote zinaelekezwa kwake.

Kiumbe cha Azhura Mazda ni asha, ukweli na mpango, ambaye anazozana na kinyume chake, druj, uongo na machafuko.

Kwa sababu binadamu ana hiari, watu lazima wawe na uwajibikaji kwa maadili wanayoyachagua. Kwa kutumia hiari, watu lazima wawe na jukumu tendaji katika mgogoro wa dunia nzima, na mawazo mema, maneno mema na matendo mema ili kuhakikisha furaha na kuepuka machafuko.

Zamani dini iliyo ilikuwa kubwa, lakini siku hizi imebaki na watu 127,000 hadi 190,000 tu.

Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uzoroastro kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.