Nenda kwa yaliyomo

Tehran

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa Tehran

Tehran (au Teheran - تهران kwa Kifarsi) ni mji mkuu wa Uajemi (Iran). Idadi ya wakazi inakadiriwa kuwa kati ya milioni 9 hadi 14.

Siku hizi mji umeenea kwenye mtelemko wa kusini wa milima ya Elburs kwenye kimo kati ya mita 1000 hadi 1700 juu ya UB. Kwa jumla mitaa maskini zaidi iko kusini ya mji katika tambarare inayoelekea jangwa la Dasht-e-kavir. Mitaa tajiri iko upande wa kaskazini kwenye mitelemko ya milima.

Tehran ilijulikana mara ya kwanza kama kijiji upende wa kaskazini wa mji wa Ray uliokuwa mji wa biashara kwenye barabara ya hariri na pia mji mkuu wa watawala juu ya sehemu za Uajemi. Baada ya kuharibiwa kwa Ray mwaka 1220 na Wamongolia Teheran ilianza kupanuka. Tangu karne ya 17 mji ulipanushwa na watawala mbalimbali na kuviringishwa na ukuta. Mwaka 1789 mfalme mpya Lotf Ali Khan wa nasaba ya Khajari alihamisha mji mkuu kutoka Shiraz kwenda Teheran iliyokuwa karibu na maeneo ya kabila yake. Mnamo mwaka 1800 mji ulikuwa na wakazi 15,000.

Mfalme aliyemfuata Fath Ali Shah (17621834) alijenga msikiti na madarsa nyingi pia ikulu ya Golestan. Mtawala Naser al-Din Shah (18311896) aliongeza eneo la mji mara tano. Mwaka 1883 Teheran ilikuwa na wakazi zaidi ya 100,000 ikawa mji mkubwa wa Uajemi.

Tangu utawala wa Reza Shah Pahlavi (1925 - 1941) barabara na reli zikajengwa Teheran ikawa kitovu cha njia za mawasialiano nchini. Mji ukaendelea kukua haraka. Reza Shah alibomoa kuta zake na kuongeza mpango wa barabara pana; yeye mwenyewe alijijengea ikuli mpya kaskazini ya mji miguuni pa milima.

Mwaka 1943 Stalin, Winston Churchill na John D. Rockefeller viongozi wa mataifa ya ushirikiano ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia walikutana hapa kwa Mkutano wa Teheran walipopatana kuhusu mipango yao ya vita.

Chini ya utawala wa Mohammad Reza Pahlavi katika miaka ya 1960 na 1970 barabara ziliendelea kupanushwa na karahani nyni kujengwa. Mji ukaendelea kukua; mwaka 1966 walikuwepo wakazi milioni 2.7, mwaka 1876 walikuwepo tayari milioni 4.5.

Wakati wa vita ya Iraq dhidi Uajemi (1980-1998) mji ulishambuliwa kwa makombora ya kiiiraqi lakini hazikuweza kusimamisha upanuzi wa mji. Leo hii idadi ya wakazi inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 10.

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tehran kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.