Kiajemi
(Elekezwa kutoka Kifarsi)
Jump to navigation
Jump to search
Kiajemi au Farsi (فارسی) ni lugha ya taifa ya Uajemi. Ni kati ya lugha za Kihindi-Kiajemi, ambazo tena ni kati ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Inaandikwa kwa herufi za Kiarabu ambamo herufi nne za ziadi zimeongezwa kwa kutaja sauti zizizoweza kuonyeshwa kwa Kiarabu asilia. Hizi herufi za ziada ni پ p, , چ tsh, ژ zh na گ ɡ.
Kiajemi ilikuwa na athira kubwa juu ya lugha mbalimbali hasa Kiarabu na Kituruki.
Inatumiwa hasa katika nchi zifuatazo:
- Uajemi (Iran)
- Tajikistan
- Afghanistan
Kuna wasemaji wa lugha ya kwanza milioni 70, na takriban wasemaji wengine milioni 60 kama lugha ya pili.
- Katika Afghanistan yenye wasemaji takriban milioni 15 lugha inaitwa "dari" (درى).
- Katika Tajikistani yenye wasemaji milioni 15 pia lugha inaitwa "Kitajiki".
Kutokana na uhamiaji wa karne ya 20 lugha inapatikana katika nchi nyingi za dunia.