Afghanistan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
د افغانستان اسلامي جمهوریت
Da Afġānistān Islāmī jomhoriyat
جمهوری اسلامی افغانستان

jomhoriye-e Eslāmī-ye Afġānistān
Jamhuri ya Kiislamu ya Afghanistan
Bendera ya Afghanistan Nembo ya Afghanistan
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: hakuna
Wimbo wa taifa: Soroud-e-Melli
Lokeshen ya Afghanistan
Mji mkuu Kabul
34°31′ N 69°08′ E
Mji mkubwa nchini Kabul
Lugha rasmi KiPashto, KiFarsi
Serikali Jamhuri ya Kiislamu
Hamid Karzai
Ahmad Zia Massoud na Karim Khalili
Uhuru
Tarehe
Kutoka Uingereza
19 Agosti 1919
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
647,500 km² (40)
N/A
Idadi ya watu
 - 2005 kadirio
 - 1979 sensa
 - Msongamano wa watu
 
29,863,000 (38th)
13,051,358
46/km² (150th)
Fedha Afghani (Af) (AFN)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+4:30)
(UTC+4:30)
Intaneti TLD .af
Kodi ya simu +93

-Afghanistan (pia: Afuganistani)ni nchi katika bara la Asia. Inapakana na nchi za Pakistan, Uajemi, Turkmenistan, Usbekistan na Tajikistan na China. Mji mkuu ni Kabul.

Ni nchi ya milima mirefu mingi inayofunika 3/4 za uso wake. Kutokana na tabia ya nchi wakazi wengi huishi katika jumuiya za kikabila.

Historia

Afghanistan kama nchi ya pekee ilianza kutokea wakati wa karne ya 19. Kabla ya hayo nchi yote au sehemu mbalimbali zilikuwa sehemu ya milki jirani hata kama sehemu za eneo la Afghanistan zilijitegemea chini ya watawala wadogo. Kwa vipindi virefu vya historia Afghanistan ilikuwa sehemu ya milki za Uajemi (Iran).

Tangu miaka ya 1980 Afghanistan imekabiliwa na vita; 1979 Umoja ya Kisovyeti ilivamia nchi ikapaswa kujiondoa tena mwaka 1979. Vita ya wenyewe kwa wenyewe ilifuata kati ya vikundi vya wapinzani ambako nchi jirani ya Pakistan ilikuwa na athira kubwa kwa kutuma silaha na pesa.

Baada ya kipindi kifupi cha serikali ya kitafai kundi la kiislamu la Taliban lilifaulu kuteka Kabul kwa msaada kutoka Saudia na Pakistan mwaka 1997.

Serikali ya Taliban ilikwisha kwa sababu walimruhusu Osama bin Laden kuwa na kimbilio nchini pamoja na kundi lake la Al-Qaide. Baada ya Shambulio la 11 Septemba 2001 Marekani ililipa kisasi kwa kushambulia Afghanistan.

Hali ya vita imeendelea ndani ya Afghanistan katika vita ya Marekani na NATO 2001-2014. Tangu Disemba 2014 nchi za NATO zilitangaza ya kwamba wamemaliza kuhudhuria katika mapigano na kuondoa sehemu kubwa ya wanajeshi kutoka Afghanistan. Vikosi vya NATO vimebakikwa shabaha ya kusidia jeshi la kitaifa.

Viungo vya nje

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.


BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Afghanistan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.