Vietnam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Cộng hòa Xã hội Chủ nghĩa Việt Nam
Jamhuri ya Kijamaa ya Vietnam
Bendera ya Vietnam Nembo ya Vietnam
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Độc lập – Tự do – Hạnh phúc
(Uhuru, Huria, Heri)
Wimbo wa taifa: Tiến Quân Ca
Lokeshen ya Vietnam
Mji mkuu Hanoi
21°2′ N 105°51′ E
Mji mkubwa nchini Mji wa Ho Chi Minh (Saigon)
Lugha rasmi Kivietnam
Serikali Jamhuri, chama kimoja 1
Nông Đức Mạnh
Nguyễn Minh Triết
Nguyễn Tấn Dũng
Uhuru
Kutoka China
(mapigano ya Bach Dang)
Kutoka Ufaransa
Ilitambuliwa

938

2 Septemba 1945
1954
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
332,698 km² (ya 65)
6.4
Idadi ya watu
 - Julai 2014 kadirio
 - 1999 sensa
 - Msongamano wa watu
 
90,630,000 (ya 13)
76,323,173
273.11/km² (ya 46)
Fedha Dong ya Vietnam (₫) (VND)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+7)
(UTC+7)
Intaneti TLD .vn
Kodi ya simu +84

-Vietnam (Việt Nam) ni nchi ya Asia ya Kusini-Magharibi.

Imepakana na China, Laos na Kambodia.

Mji mkuu ni Hanoi lakini mji mkubwa ni Mji wa Ho Chi Minh (zamani: Saigon).

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Umbo la nchi ni kama kanda ndefu kando ya mwambao wa Bahari ya Kusini ya China. Umbali kati ya kaskazini na kusini ni km 1,650. Upana wa nchi kati ya mashariki na mipaka ya magharibi hutofautiana: kaskazini ni km 600, lakini kwenye shingo jembamba la Vietnam ya kati ni kilomita 50 tu. Pwani ina urefu wa km 3,000.

Kidaka cha Halong katika Vietnam Kaskazini

Umbo la kijiografia limewahi kulinganishwa na "fimbo linalobeba mabakuli mawili": kaskazini na kusini kuna delta mbili ya mto Mekong na Mto Mwekundu zenye rutuba; katikati nchi nyembamba ya milima na misitu.

Kuna maeneo makubwa matano:

Historia[hariri | hariri chanzo]

Milki jirani ya China[hariri | hariri chanzo]

Vietnam ilitawaliwa kwa karne kadhaa kutoka China. Athira ya kiutamaduni ya China ilibaki muhimu hata katika uhuru.

Katika karne ya 18 nchi iliunganishwa chini ya makaisari wa Hue.

Koloni la Ufaransa[hariri | hariri chanzo]

Athira ya Ufaransa ilikua na kati ya miaka 1858 na 1883 utawala wa nchi ulichukuliwa na Ufaransa. Kusini mwa nchi kulikuwa koloni la Ufaransa kwa jina la Cochinchina. Annan (eneo la Vietnam ya Kati) na Tongking (kaskazini) zilikuwa nchi lindwa chini ya utawala wa kaisari wa Hue lakini hali halisi mamlaka ilikuwa mikononi mwa Ufaransa.

Hekalu la Kibuddha

Vita ya ukombozi[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Vietnam ilitwaliwa na Japani iliyoacha maafisa Wafaransa wa serikali ya Víchy ofisini lakini kushika utawala wa juu.

Kundi la Viet Minh walioongozwa na mkomunisti Ho Chi Minh waliwapinga kwa njia ya vita ya msituni.

Mwaka 1945 Japani ilijaribu kutumia Wavietnam upande wake ukaondoa Wafaransa madarakani na kumtangaza Kaisari Bao Dai wa Hue mtawala wa Vietnam huru.

Lakini baada ya miezi michache vita ikaisha na Ho Chi Minh alitangaza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Vietnam mjini Hanoi. Wafaransa wa serikali ya Paris walijaribu kujenga uhusiano naye lakini baada ya kurudi walilenga kuchukua utawala upya.

Vita ya kupigania uhuru ilifuata hadi mwaka 1954 Ufaransa ukashindwa.

Kipindi cha Vietnam mbili[hariri | hariri chanzo]

Vietnam iligawiwa katika Vietnam Kaskazini na Vietnam Kusini. Jeshi na watawala wa kikoloni wa Ufaransa waliondoka kabisa. Wavietnam wengi wa kaskazini, hasa Wakristo, walioogopa serikali ya kikomunisti walikimbilia kusini.

Lakini uchaguzi huru uliokubaliwa huko Geneva haukutekelezwa kwa sababu serikali za kidikteta za kusini zilikataa.

Vita ya wenyewe kwa wenyewe ilianzishwa na wakomunisti wa kaskazini waliosaidiwa na China na Umoja wa Kisovyeti dhidi ya serikali ya kusini iliyopata msaada wa Marekani.

Kaskazini kuteka Kusini na kuunganisha taifa[hariri | hariri chanzo]

Katika vita ya Vietnam majeshi ya Marekani na Vietnam Kusini yalishindwa.

Tarehe 30 Aprili 1975 jeshi la Vietnam Kaskazini ilitwaa mji wa Saigon. Nchi yote iliunganishwa kama Jamhuri ya Kijamaa ya Vietnam tarehe 2 Julai 1976.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Kwa jumla kuna wakazi milioni 86.5 million.

Wengi (85.7%) ni Waviet. Wengine ni wa makabila madogomadogo 54 ambayo hakuna linalofikia 2%.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kiviet.

Upande wa dini, siasa ya ukomunisti inabana uhuru. Kadiri yake 18.2% tu za wakazi wamejiandikisha kufuata dini fulani, wakiwemo Wabuddha (7.9%), Wakatoliki (6.6%), waumini wa Hòa Hảo (1.7%), Wakaoda (0.9%) na Waprotestanti (0.9%), kumbe wengine wote hawamuamini Mungu.

Lakini utafiti kutoka nje unataja namba tofauti, hasa kwa dini za jadi, kwamba zinafuata na 45.3% za wakazi wote, na kwamba wasio na dini yoyote ni 29.6%.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Kati ya miaka 1940 na 1975 Vietnam ilikuwa na kipindi kirefu cha vita ikaonekana kama nchi maskini sana.

Tangu miaka ya 1980 uchumi umesonga mbeleː sasa ni kati ya nchi kwenye njia ya maendeleo zenye uchumi imara sana unaokua haraka.

Usafiri[hariri | hariri chanzo]

Nyanja za ndege za kimataifa ni:

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Serikali
Vyombo vya habari na uhuru wa uandishi
Utalii
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Kirgizstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Vietnam kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.