Vyombo vya habari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Vyombo vya habari mbalimbali

Vyombo vya habari ni vyombo vya mawasiliano vinavyolenga watu wengi iwezekanavyo kwa shabaha ya kuwapatia habari au burudani.

Mifano yake ni magazeti, redio, televisheni au intaneti.

Kuna wataalamu wanaojumlisha pia vitabu katika historia ya vyombo ya habari tangu kupatikana kwa uchapishaji vitabu; wengine wanaona pia aina za maigizo ya tamthiliya kama vyombo vya habari katika jamii za kale.

Kwa jumla maelezo ya kitaalamu ya vyombo vya habari ilikuwa hadi juzi:

"Mawasiliano kwa vyombo vya habari ni mawasiliano ambako habari zinasambazwa wazi (bila kuzuia au kutenga sehemu ya watu kwa kusudi) kwa njia ya mbinu za teknolojia lakini si moja kwa moja (yaani kupitia umbali) na kutoka upande mmoja (watoa habari na wapokeaji hawabadilishani nafasi zao) kwa wapokeaji waliosambazwa." [1]

Iko wazi ya kwamba tamthiliya haikubaliki na maelezo haya. Lakini tangu kupatikana kwa intaneti hasa Web 2.0 tofauti kati ya watoa habari na wapokeaji imeshaanza kuondolewa kwa mfano kwa njia ya blogu na mitandao ya kijamii.

Vyombo vya habari vya kwanza kwa maana iliyoelezwa juu vilikuwa magazeti. Yalifuatwa na redio na baadaye televisheni. Katika miaka ya kwanza ya sinema filamu fupi za habari zilizoonyeshwa kabla ya filamu kuu zilikuwa pia chombo muhimu cha habari kwa umma.

  1. Gerhard Maletzke: Psychologie der Massenkommunikation. In: Ders.: Kommunikationswissenschaft im "Uberblick. Opladen usw. 1998; 45 f.
Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vyombo vya habari kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.