Televisheni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
TV ya Kijerumani ya mwaka wa 1956.

Televisheni au runinga (pia: TV, telly au tyubu) ni chombo (kifaa) chenye kiwambo au kioo ambacho kinapokea mawasiliano kutoka katika kituo cha televisheni na kuyabadilisha kuwa picha na sauti. Neno "televisheni" linatokana na neno tele (kutoka Kigiriki: kwa mbali sana) na Kilatini vision (kuona), kwa pamoja inaunda neno tele-visheni.

Historia ya televisheni[hariri | hariri chanzo]

TV Braun HF 1 ya Kijerumani ya mwaka wa 1959.

Kikawaida TV inaonekana kama sanduku. TV za zamani kabisa zilikuwa zina kirimba au fremu kubwa ya mbao na zilikuwa zikiwekwa chini kama fanicha. TV za kisasa ziko za namna nyingi kama zilivyo nyingi zaidi. Kuna baadhi ya TV zinaweza kunea mkononi mwako na zikawa zinaendeshwa kwa kutumia mabeteri.

TV zingine zinaweza kuenea ukuta mzima wa nyumba, na inaweza kukaa katika sakafu, au kuna zingine ambazo zimenyooka (flat) na zinaweza kubandikwa ukutani. Televisheni inaweza kuonyesha picha kutoka sehemu mbalimbali. Cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kutumia kidaka mawasiliano au antenna (au aerial), hii itaonyesha maonyesho yote yanayorushwa na kituo cha matangazo ya televisheni.

Vituo vya TV vinaweza kuwa mbali kabisa lakini bado matangazo yake yanapatikana kama antena ya kurusha mawimbi yake iko katika umbali wa kilomita 50 hadi 150. Teknolojia mpya zaidi ni kutumia vyombo vya angani kama antena ya kurusha mawimbi haya duniani. TV pia inaweza kuonyesha filamu kutoka katika VCD na DVD au VCR yaani tepu za kawaida. Cable TV na Satellite TV zinaweza zikatoa huduma nyingi ya vipindi vya TV kwa mara moja na vilevile kuvirusha hewani. Michezo mingi ya Video huunganishwa katika TV ili uweze kuona kile unachokicheza. Kuna baadhi ya tarakilishi au kompyuta ambazo unaweza kutumia TV kama kioo cha kufanyia kazi zako (kiwambo) au kwa jina lingine monitor.

TV zote zina kiwambo ambacho kinaonyesha picha. Kabla ya miaka ya 1970 TV zilikuwa hazina rangi ( yaani "black and white"), ambazo zilikuwa zinafanya kila kitu kionekane cha rangi ya kijivu. Lakini kwa sasa karibuni TV zote zinaonyesha na rangi. Kawaida ya viwambo vingi (kioo au vioo) vingi huonyesha kuwa vina kona ya mzunguko, lakini kwasasa vioo vingi hutengenzwa kwa kunyooka na zina ncha pembeni.

Njia ya picha katika TV

Kabla ya miaka ya 1990, TV zote zilikuwa zikitengenezwa kwa umbo moja-zilikuwa kubwa kidogo na kisha zilikuwa ndefu. Kwa mfano, kama kioo kilikuwa cha urefu wa inchi 3, basi lazima kitakuwa na upana wa inchi 4. Au kama kioo kina urefu wa cm 30, lazima kitakuwa kina upana wa cm 40.

Umbo la TV za kisasa linazidi kuwa maarufu na kupata wapenzi wengi zaidi kila siku ziendapo. TV zenye kioo cha upana mkubwa wa mstatili huonekana vizuri katika runinga kubwa (theatre screen) na pia inapendeza wengi zaidi. Hizi huziita kioo kipana (au kwa kiing: widescreen). Endapo TV ya kioo kipana ina urefu wa cm 30, basi lazima itakuwa ina upana wa cm 53. Ili ifanye kazi vizuri, uonyeshaji wa TV pia unatakiwa ujengwe kwa namna ya upana yaani 'widescreen'. Kioo kipana kinaweza kubadilishika kwa ukubwa wowote unaoutaka, lakini swala la umbo linabaki kuwa vilevile kama lilivyo (Widescreen).

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: