Nenda kwa yaliyomo

Inchi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Inchi (kutoka Kiingereza inch) ni kipimo cha urefu wa sentimita 2.54. Inatumika pamoja na futi na maili. Si kipimo sanifu cha kimataifa SI bali ni kizio cha vipimo vya Uingereza.

Asili yake ni upana wa kidole gumba cha mtu. Kwa hiyo inchi inalingana takriban na wanda kati ya vipimo asilia vya Kiswahili ambayo ni pia kipimo cha upana wa kidole ingawa haikusanifishwa.

  • inchi 1 = millimita 25.4
  • inchi 12 = futi 1 = millimita 304.8
  • mita 1 = takriban inchi 39.37

Kifupi chake inchi ni: "futi 5 inchi 11 = 5' 11".

Kipimo cha inchi kiliingia katika Kiswahili tangu ukoloni wa Uingereza.

Kihistoria urefu wa inchi ulikuwa tofauti kati ya nchi na nchi. Leo hii inatumiwa zaidi Marekani lakini pia kwa mazoea katika nchi zinazotumia sana lugha ya Kiingereza hata kama wameshahamia vipimo sanifu vya kimataifa SI.

Mafundi hutumia inchi wakipima unene wa bomba la maji au wa ubao uliokatwa.