Wanda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wanda mmoja.
Wanda.

Wanda (wingi: "nyanda") ni kipimo cha urefu kinacholingana na upana wa kidole kimoja au karibu inchi moja. Vipimo vya kufanana vilitumiwa katika nchi na tamaduni mbalimbali kwa kutumia upana wa kidole gumba.

Ni kati ya vipimo asilia vya Kiswahili, si kipimo sanifu cha kisasa.

Wanda kama "dimension"[hariri | hariri chanzo]

Katika lugha ya sayansi kuna jaribo la kutumia "wanda" pia kwa pande za ulimwengu wetu kama neno la Kiingereza "dimension"[1].

Kwa maana hiyo mstari una wanda mmoja, eneo kama mraba au mviringo huwa na nyanda mbili, gimba kama mchemraba au tufe huwa na nyanda tatu.

Ulimwengu mara nyingi huelezwa kuwa na nyanda nne, yaani urefu, upana, kimo na wakati.

Istilahi mbadala inayotumiwa kama jaribio kwa kutaja jambo lilelile ni pandeolwa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. linganisha KAST 1995, uk 354
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wanda kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.