Nenda kwa yaliyomo

Vipimo sanifu vya kimataifa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kipimo sanifu cha kisasa)
Vizio vya kimsingi vya SI
Alama Jina Inataja
s sekunde wakati
m mita urefu
kg kilogramu masi
A ampea mkondo wa umeme
K kelvini halijoto
mol moli kiasi cha dutu
cd kandela mwangaza

Vipimo sanifu vya kimataifa (kwa ing. International system of measurements, kwa far.: Système International d'unités; kifupi chake: SI) ni utaratibu uliokubaliwa kimataifa kwa kuwa na vizio vya upimaji vya pamoja duniani. Maendeleo na matumizi ya utaratibu huo huangaliwa na Ofisi ya Kimataifa ya Vipimo.

Mfumo huu unatumia vizio saba vya kimsingi pamoja na viambishi awali 20 kwa kutaja vigawe au sehemu za vizio hivi katika mfumo wa viambishi awali vya vipimo sanifu vya SI.

Vizio vya kimsingi ni:

Vizio vyote vingine kama vile eneo, kani, shinikizo au ukinzani kiumeme vinatokana na vizio asilia.

Vipimo hivi hutumika na wanasayansi kote duniani vimeenea pia katika bishara na ufundi. Hata hivyo katika maisha ya kawaida kuna vipimo mbalimbali vinavyoweza kuwa tofauti kati ya nchi na nchi.

Tazama pia