Vipimo sanifu vya kimataifa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Vipimo sanifu vya kimataifa (ing. International system of measurements, far.: Système International d'unités; kifupi chake: SI) ni utaratibu uliokubaliwa kimataifa kwa kuwa na vizio vya upimaji vya pamoja duniani. Maendeleo na matumizi ya utaratibu huo huangaliwa na Ofisi ya Kimataifa ya Vipimo.

Mfumo huu unatumia vizio saba vya kimsingi pamoja na viambishi awali 20 kwa kutaja vigawe au sehemu za vizio hivi katika mfumo wa viambishi awali vya vipimo sanifu vya SI.


Vizio vya kimsingi ni:

Vizio vyote vingine kama vile eneo, shinikizo au ukinzani kiumeme vinatokana na vizio asilia.

Vipimo hivi hutumika na wanasayansi kote duniani vimeenea pia katika bishara na ufundi. Hata hivyo katika maisha ya kawaida kuna vipimo mbalimbali vinavyoweza kuwa tofauti kati ya nchi na nchi.


Tazama pia[hariri | hariri chanzo]