Kelvini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
CelsiusKelvinThermometer.jpg

Kelvini ni kipimo cha SI kwa halijoto. Alama yake ni K.

Kiwango chake kinaanza kwenye sifuri halisi (= -273.15 °C) pasipo na mwendo wowote wa molekuli. Kizio kimoja cha Kelvini ni sehemu ya 1/273.16 ya tofauti kati ya sifuri halisi (=0 K) na kiwango utatu cha maji (+0.01 °C).

Skeli ya Kelvini ililinganishwa na skeli ya selsiasi yaani kizio kimoja cha Kelvini ni sawa na kizio kimoja cha Selsiasi. Skeli ya Kelvini haihitaji namba za minusi (-) kwa sababu hakuna hali chini ya 0 K.

Jina limetokana na mwanafisikia Mwingereza William Thomson aliyekuwa na cheo cha Lord Kelvin (1824–1907).


Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kelvini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.