Namba hasi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kipimajoto kikionyesha joto hasi la Fahrenheit (−4°F).

Namba hasi katika hisabati ni namba halisi ambayo ni pungufu ya namba 0.

Namba hasi huwakilisha kinyume. Kama namba chanya inawakilisha elekea kulia, namba hasi inamaanisha elekea kushoto. Kama namba chanya inawakilisha juu ya usawa wa bahari, basi namba hasi itwakilisha chini ya usawa wa bahari. Kama namba chanya inawakilisha kuweka, namba hasi inawakilisha kutoa. Mara nyingi huwakilisha ukubwa wa deni au upungufu.

Mstari wa namba hasi na namba chanya.