Nenda kwa yaliyomo

Namba halisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alama ya kundi la namba halisi ni (ℝ).
Namba halisi zinaweza kuwa kama pointi katika mstari wa tarakimu.

Namba halisi (kwa Kiingereza: "Real numbers") katika hisabati ni thamani inayowakilisha kiasi katika mstari wa kuendelea. Kivumishi halisi kwa mantiki hii kilianzishwa kwenye karne ya 17 na Mfaransa Descartes, ambaye alitofautisha namba halisi na namba changamano.

Namba halisi zinajumuisha namba wiano, kama vile nambakamili −5 na sehemu 4/3, na namba zisizowiani, kipeo cha pili cha 2, na aljebra). Ikijumuisha na zisizowiani ni namba zisizo na mwisho, kama pai (3.14159265…).

Namba halisi zinaweza kuwa kama pointi katika mstari mnyoofu unaoitwa mstari wa tarakimu au mstari halisi, ambapo pointi za namba halisi ambazo zimeachiana nafasi sawa.

Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Namba halisi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.