Nenda kwa yaliyomo

Kifaransa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Far.)
Kifaransa
Français (fr)
Lugha
Asili Ufaransa, Ubelgiji, Uswisi, Monako, Kanada
Wasemaji

L1 : 74 Milioni
L2: 238 Milioni

Jumla: 310 Milioni
Familia za lugha Kihindi-Kiulaya
Kilatini
Kifaransa cha Kale
Aina za Awali Kilatini cha Kale
Kilatini Halisi
Kifaransa cha kale
Kifaransa cha Kati
Mfumo wa kuandika Kilatini
Lugha Rasmi
Lugha rasmi kwa Nchi 29
Nambari za Msimbo
ISO 639-1 fr
ISO 639-2 fra
Glottolog stan1290

     Lugha ya Kwanza kwa wengi      Lugha rasmi au ya kwanza kwa wachache      wachache wanazungumza

Kifaransa ni lugha ya Kirumi iliyotokana na Kilatini na kuendelezwa katika eneo la Gallia, ambalo ni Ufaransa ya sasa. Ni moja ya lugha zinazozungumzwa zaidi duniani, ikiwa na takriban wasemaji milioni 300, wakiwemo wazungumzaji wa asili na wale wa lugha ya pili. Kifaransa ni lugha rasmi ya Ufaransa na mataifa kadhaa, hasa barani Afrika, Ulaya, Karibi, na sehemu za Asia na Amerika Kaskazini. Pia ni moja ya lugha sita rasmi za Umoja wa Mataifa na inatumika sana katika diplomasia, mashirika ya kimataifa, na fasihi.

Lugha ya Kifaransa ilitokana na Kilatini cha Kawaida, ikichanganyikana na lugha za Kikelti na Kijerumaniki (Kifranki) zilizozungumzwa katika Gaul. Katika Enzi za Kati, iliendelea kuwa Kifaransa cha Kale, kisha Kifaransa cha Kati, na hatimaye Kifaransa cha Kisasa. Akademia ya Kifaransa, iliyoanzishwa mwaka 1635, inasimamia na kuhakikisha usanifishaji wa lugha. Kifaransa kinajulikana kwa sarufi yake changamano, msamiati wake mpana, na vokali zinazotamkwa kwa njia ya pua. Kutokana na historia ya ukoloni wa Ufaransa, Kifaransa kimeendelea kuwa lugha kuu katika makoloni ya zamani, hasa barani Afrika, ambako kinatumika kama lugha rasmi au ya kiutawala katika nchi nyingi.

Wasemaji

[hariri | hariri chanzo]

Takwimu kuhusu matumizi ya Kifaransa hutofautiana. Kadirio ndogo lasema kuna watu milioni 87 wanaotumia Kifaransa kama lugha ya kwanza, na tena milioni 100 wanaoitumia kama lugha ya pili. Kadirio kubwa lataja milioni 112,6 wasemaji wa lugha ya kwanza pamoja na milioni 60,6 wenye uwezo wa kutumia Kifaransa karibu kama lugha ya Mama. Halafu hutajwa takriban milioni 100 - 110 wanaotumia Kifaransa kikazi, kibiashara au masomoni jumla takriban milioni 300 wasemaji wa Kifaransa duniani.

Historia ya lugha

[hariri | hariri chanzo]

Kifaransa ni kati ya lugha za Kirumi. Asili yake ni Kilatini lugha ya Waroma wa Kale. Hadi mwaka 50 KK watu waliokalia Gallia (eneo la Ufaransa wa leo) walitumia lugha mbalimbali za Kikelti. Baada ya uvamizi na Waroma Gallia ilikuwa sehemu ya Dola la Roma. Lugha ya Kilatini ilienea hadi kuwa lugha ya watu wengi. Kikelti kimebaki hadi leo katika maeneo madogo kama Ubritani.

Kilatini hiki jinsi kilivyojadiliwa na watu wa kawaida katika Gallia kilipokea kiasi cha maneno na matamshi na lugha ya Kikelti. Baada ya mwisho wa Dola la Roma lugha iliendelea kubadilika haraka zaidi. Makabila ya Kigermanik walivamia Gallia na kuleta athira ya lugha zao.

Haya yote yaliunda lugha ya Kifaransa ambayo ni lugha karibu sana na Kilatini hivyo pia na lugha kama Kiitalia, Kihispania na Kireno.

Kifaransa kilichokuwa rasmi kilifuata lahaja ya eneo la Paris. Tangu 1634 kuna Akademia ya Kifaransa aabayo ni taasisi ya kulinda usafi wa lugha.

Kifaransa kilienea kimataifa kwa sababu Ufaransa ilikuwa taifa lenye maendeleo mengi katika Ualya. Kifaransa kilikuwa katika nchi nyingi lugha ya elimu na pia ya mawasiliano ya kimataifa jinsi ilivyo siku hizi Kiiingereza mahali pengi.

Baada ya Ufaransa kuwa nchi yenye koloni lugha ilisambazwa hata nje ya Ulaya. Ubelgiji yenye Kifaransa kama lugha rasmi ilikuwa pia na koloni na kupeleka lugha huko.

Hali ya Lugha kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Kifaransa ni lugha ya kitaifa, lugha rasmi, lugha ya utawala au lugha ya mawasiliano katika nchi zifuatazo:

  • Lugha ya kitaifa pamoja na lugha nyingine
Luxemburg
Ubelgiji (lugha rasmi hasa katika jimbo la Wallonia)
Uswisi (lugha rasmi hasa katika mikoa ya magharibi)
  • Lugha rasmi kimkoa
Italia katika mkoa wa Val d'Aoste

Lugha rasmi ya nchi zifuatazo

  • Lugha ya utawala:
Jibuti
Mauritania
  • Lugha ya elimu na mawasiliano, lakini wala lugha ya kitaifa wala lugha rasmi katika
Aljeria
Moroko
Tunisia

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]