Eneo la ng'ambo la Ufaransa
Mandhari
(Elekezwa kutoka Eneo la ng’ambo la Ufaransa)
Maeneo ya ng'ambo ya Ufaransa ni maeneo nje ya Ulaya zilizokuwa koloni lakini zimeendelea kuwa sehemu za Ufaransa.
Hali ya kisheria
[hariri | hariri chanzo]Maeneo haya hutofautiana katika hali ya kisheria lakini wakazi wao wote ni raia wa Ufaransa na kila eneo linachagua wabunge wake kwa bunge la Paris. Isipokuwa maeneo yasiyokaliwa na watu hawana mbunge.
- mengine ni mikoa (departement) kamili sawa na mikoa mingine ndani ya Ufaransa bara; maeneo yao ni sehemu ya Umoja wa Ulaya.
- mengine ni jumuiya za kujitawala (collectivite) chini ya Ufaransa; hazihesabiwi kuwa sehemu za Umoja wa Ulaya; zinajitwala katika mambo ya ndani lakini mambo ya nje, jeshi na sheria huendeshwa na serikali ya kitaifa na sheria za bunge la Paris.
- kuna bado eneo moja la ng'ambo linalotawaliwa na serikali ambalo ni visiwa vya kusini vya Kifaransa katika Bahari Hindi.
Mikoa ya Ng'ambo (Département d'outre-mer) au Jimbo la Ng'ambo (Région d'outre-mer)
[hariri | hariri chanzo]- Guadeloupe (tangu 1946 - Bahari ya Karibi)
- Martinique (tangu 1946 - Bahari ya Karibi)
- Guyana ya Kifaransa (tangu 1946 - Amerika ya Kusini)
- Réunion (tangu 1946 - Bahari Hindi)
- Mayotte katika Bahari Hindi karibu na Komori; mwaka 2011 wakazi walipiga kura wakaamua kuendelea kama Mkoa wa Ng'ambo (Département d'outre-mer).
Eneo la Ng'ambo (Territoire d'outre-mer)
[hariri | hariri chanzo]- Visiwa vya kusini vya Kifaransa katika Bahari Hindi tangu 1956)
Jumuiya za Kujitawala za Ng'ambo Collectivité d'outre-mer
[hariri | hariri chanzo]Jumuiya hizi zilianzishwa kwa mabadiliko ya katiba ya Ufaransa mwaka 2003. Kila jumuiya imeundwa kwa sheria ya pekee.
- Polynesia ya Kifaransa katika Bahari ya Pasifiki.
- Saint Pierre na Miquelon katika Atlantiki karibu na Kanada.
- Wallis na Futuna katika Pasifiki ya kusini
Nouvelle-Calédonie au Kaledonia Mpya
[hariri | hariri chanzo]- Kaledonia Mpya (katika Pasifiki ya kusini) ni eneo la pekee; sehemu ya wakazi wanadai uhuru na kati ya 2014 na 2019 wakazi wote watapiga kura kuhusu swali la kubaki na Ufaransa au kuanzisha nchi huru.
Visiwa visivyokaliwa na watu
[hariri | hariri chanzo]Ufaransa hutawala au kudai utawala juu ya visiwa vidogovidogo bila wakazi:
Bahari Hindi
[hariri | hariri chanzo]Visiwa hivi hudaiwa pia na Madagaska na Tromelin inadaiwa na Shelisheli.
Pasifiki
[hariri | hariri chanzo]- Kisiwa cha Clipperton
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Official site Ilihifadhiwa 12 Oktoba 2005 kwenye Wayback Machine.
- past and current developments of France's overseas administrative divisions like pays d'outre-mer (French language) Ilihifadhiwa 29 Septemba 2006 kwenye Wayback Machine.