Nenda kwa yaliyomo

Wallis na Futuna

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Wallis na Futuna baharini.

Wallis na Futuna ni eneo la ng’ambo la Ufaransa liloko katika Bahari ya Pasifiki Kusini, kati ya Fiji na Samoa. Inajumuisha makundi mawili ya visiwa vikuu, Wallis (Uvea) na Futuna, pamoja na visiwa vidogo kadhaa. Eneo hili lina idadi ya wakazi takriban 11,000, likiwa miongoni mwa maeneo yenye idadi ndogo zaidi ya watu ulimwenguni. Kwa jumla, lina eneo la kilomita za mraba 142, na ni mojawapo ya maeneo madogo zaidi ya Ufaransa. Mata-Utu, iliyoko katika Kisiwa cha Wallis, ndiyo mji mkuu na mji mkubwa zaidi wa eneo hili.

Wakazi walio wengi ni Wapolynesia wakiongea lugha za Kipolynesia pamoja na Kifaransa.

Wakazi walio wengi huishi kwa kilimo cha kujikimu. Uchumi hutegemea misaada kutoka Ufaransa. Katika miaka iliyopita utalii umeanza kuchangia katika pato.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.