Shirikisho la Mikronesia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Federated States of Micronesia
Bendera ya Mikronesia Nembo ya Mikronesia
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa:
Wimbo wa taifa: Patriots of Micronesia
Lokeshen ya Mikronesia
Mji mkuu Palikir
6°55′ N 158°9′ E
Mji mkubwa nchini Weno
Lugha rasmi Kiingereza (kitaifa), Kiulithi, Kiwoleai, Kiyap, Kipohnpei, Kikosrae na Kichuuk (kijimbo)
Serikali Jamhuri
David W. Panuelo
Uhuru
Tarehe
3 Novemba 1986
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
702 km² (ya 177)
Idadi ya watu
 - Julai 2019 kadirio
 - 2000 sensa
 - Msongamano wa watu
 
104,468 (ya 198)
107,000
158.1/km² (ya 75)
Fedha US Dollar (USD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+10)
(UTC-)
Intaneti TLD .fm
Kodi ya simu +691

-


Shirikisho la Mikronesia ni nchi ya visiwani katika Bahari Pasifiki iliyoko kaskazini kwa Papua Guinea Mpya.

Ni nchi huru inayoshirikiana na Marekani. Nchi ilikuwa eneo lindwa chini ya Marekani kwa niaba ya Umoja wa Mataifa hadi ikapata uhuru wake mwaka 1986.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Shirikisho linajumlisha sehemu kubwa ya funguvisiwa la Karolini katika Mikronesia, kanda la Pasifiki. Jumla ya visiwa ni 607.

Nchi ina majimbo manne ya kujitawala ambayo ni Chuuk, Kosrae, Pohnpei na Yap.

Visiwa vya Palau pia ni sehemu ya Karolini lakini ni nchi ya pekee.

Mji mkubwa wa nchi ni Weno (wakazi 17,624) kisiwani Chuuk lakini mji mkuu ni Palikir kwenye kisiwa cha Pohnpei.

Majimbo ya shirikisho[hariri | hariri chanzo]

Kuna majimbo manne kama yafuatayo:

Bendera Jimbo Mji Mkuu Eneo la nchi kavu[1] Wakazi[2] Msongamano
Flag of Chuuk Chuuk Weno 127 km2 53,595 1,088 per km2
Flag of Kosrae Kosrae Tofol 110 km2 7,686 70 per km2
Pohnpei Palikir 346 km2 34,486 100 per km2
Flag of Yap Yap Colonia 118 km2 11,241 95 per km2

Historia[hariri | hariri chanzo]

Map of the Federated States of Micronesia CIA.jpg

Visiwa vimekaliwa na watu tangu miaka 4,000 iliyopita, hasa kutoka Rasi ya Malay na visiwa vya Indonesia. Wengine wametokea visiwa vya Polinesia.

Kisiwani Yap kulitokea dola na utawala wa kifalme.

Tangu kufika kwa Wahispania katika karne ya 16 visiwa vilikuwa chini ya ubwana wa nje lakini maisha ya kawaida yaliendelea bila mabadiliko makubwa kwa muda mrefu.

Mwisho wa karne ya 19 Hispania iliuza koloni hilo kwa Ujerumani; utawala wa Kijerumani ulikwisha katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ukachukuliwa na Japani hadi mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Japani ilifuatwa na Marekani iliyoendelea kutawala kwa niaba ya UM hadi uhuru.

Lugha na utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Kanisa katoliki kisiwani Pohnpei

Kuna lugha 18 ambazo huzungumzwa katika Shirikisho la Mikronesia. Lugha rasmi ni Kiingereza.

Wakazi wengi ni wa makabila ya asili.

Upande wa dini, wengi ni Wakristo (95.3%), kwanza Wakatoliki (52.6%) halafu Waprotestanti wa madhehebu mbalimbali (41.7%).

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Uchumi wa nchi hutegemea hasa kilimo cha kujisukuma na uvuvi. Mapato ya serikali ni kutokana na vibali kwa wavuvi wa nje wanaovua samaki ndani ya maji ya shirikisho.

Kuna pia uchimbaji wa fosfeti.

Shirikisho la Mikronesia pamoja na Nauru vinaongoza duniani kwa asilimia kubwa ya watu wanene.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. FSM government website - Geography. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2007-04-07.
  2. FSM government website - Population. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-06-29. Iliwekwa mnamo 2007-04-07.


Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.